TAZAMA PICHA:-Duka la MSD wilayani Chato/Geita Lafunguliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 18, 2016

TAZAMA PICHA:-Duka la MSD wilayani Chato/Geita Lafunguliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato,mkoani Geita,March 16,2016..

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw.Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(Tamisemi) mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua duka la dawa la MSD Wilayani Chato March 16,2016.

Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad