![]() |
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - EAST
AFRICA
SAUTI SOL WAACHIA HIGHER-HAIYA! –
WIMBO MPYA WA KITAIFA MAHSUSI KWA STAFTAHI (KIFUNGUA KINYWA)
Kundi la muziki la nchini Kenya
lililoshinda tuzo mbalimbali, Sauti Sol, limeachia wimbo maalum wa
kitaifa kwa ajili ya kusindikiza staftahi (kifungua kinywa) kwa ushirikiano na
kampuni ya Unilever Kenya.
HIGHER-HAIYA! Ni wimbo halisi wa kuchezeka
wenye ujumbe mzito wa kutuhamasisha sote. Wimbo umetumbuizwa na Sauti Sol na
umeandikwa na wao wenyewe wakishirikiana na Tim Rimbui na
kurekodiwa/kutayarishwa na Tim ‘Timwork’ Rimbui wa Ennovatormusic.
“Wimbo ni mzuri na ni ukumbusho
mwingine kwamba mwanzo mzuri ni kiashirio cha kwanza cha mwisho wake.
Ni muhimu
kwamba staftahi inatayarishwa kwaajili ya washindi; kwanza tunakuwa hivi
tulivyo kwa kile tulichofunguliwa kinywa asubuhi na siku njema huanza asubuhi,”
yamesema maelezo ya Sauti Sol.
Upate wimbo HIGHER-HAIYA! na
artwork yake kwenye ambatanisho la email hii. Kuwa huru kusambaza uwezavyo
kwenye mitandao unayoitumia.
Upate HIGHER-HAIYA! kwenye Waabeh
buree: http://waabeh.com/unilever/higherhaiya
Kwa maelezo zaidi: Fuata kwenye Twitter @BlueBandKenya #GoodBreakfastChallenge
MAELEZO MUHIMU KWA WAHARIRI
Februari 2016, Sauti Sol
walizindua santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika jijini Nairobi kama
sehemu ya ziara yao ya kitaifa ya mwaka 2016 Live and Die in Afrika. Live
and Die in Afrika ilijumuishwa kwenye nyimbo 10 bora za BBC Africa kwa mwaka
2015 na albamu 15 bora za Okayafrica kwa mwaka 2015.
Walitajwa pia kwenye orodha ya
Billboard Africa kama kundi lenye mustakabali mkubwa zaidi (Most Promising
Music Group). Walitajwa kwenye gazeti la The Standard kwenye orodha ya
mwaka 2016 ya ‘Agenda Setters’ na pia kuwekwa kwenye jarida la DRUM la Afrika
Mashariki kwenye orodha ya mwaka 2015 ya Movers and Shakers.
Mwaka 2015, Sauti Sol walitengeneza
vichwa vya habari duniani baada ya kutumbuiza na kucheza na marais, Barack
Obama wa Marekani na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwenye chakula cha jioni katika
ikulu ya Nairobi.
Kwa sasa ni kundi pekee ambalo picha yake imetundikwa kwenye ikulu ya White House. Washindi hao wa MTV Europe Awards (EMA) 2014 pia walishinda tuzo ya kundi bora la muziki Afrika Mashariki kwenye tuzo za Bingwa.
Tuzo zingine walizonyakua mwaka 2015
ni pamoja na wimbo wao ‘Sura Yako’ kuwa wimbo bora wa Afrika Mashariki kwenye tuzo
za Kilimanjaro (Tanzania), kundi ambalo nyimbo zake zimepakuliwa zaidi kwenye
tuzo za Mdundo na video bora ya Kenya kwa wimbo ‘Sura Yako’ kwenye tuzo za
Bingwa (Kenya) na kundi bora barani Afrika kwenye tuzo za AFRIMMA
(Marekani) na tuzo za AFRIMA (Nigeria).
Mfollow @skytanzania kwenye
Instagram au soma makala zake mbalimbali kupitia bongo5.com
Entertainment & Music
Publicity
+254 721 368 983
"Life
shrinks or expands in proportion to one's courage." - Anais Nin
(French-Cuban Author)
|
Wednesday, March 02, 2016
Home
WASANII
SAUTI SOL WAACHIA HIGHER-HAIYA:-Ni Wimbo Mpya wa Kitaifa Mahususi kwa Staftahi (KIFUNGUA KINYWA)
SAUTI SOL WAACHIA HIGHER-HAIYA:-Ni Wimbo Mpya wa Kitaifa Mahususi kwa Staftahi (KIFUNGUA KINYWA)
Tags
# WASANII
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
WASANII
Labels:
WASANII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment