MSANII WA NIGERIA:-RAVE na Video ya Wimbo ‘TONIGHT’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 02, 2016

MSANII WA NIGERIA:-RAVE na Video ya Wimbo ‘TONIGHT’

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - EAST AFRICA

MSANII WA NIGERIA – RAVE AACHIA WIMBO NA VIDEO MPYA YA ‘TONIGHT’

Cadilly Entertainment wanamleta kwako msanii wa Nigeria,  Wilfred Utere, anayejulikana zaidi kwa mashabiki wake kwa jina la Rave akiwa na kazi yake mpya, iitwayo TONIGHT.

Mtumbuizaji huyo mwenye vipaji vingi vikiwemo uchezaji dansi na anajulikana zaidi kwa kushinda shindano la kucheza muziki la Nigeria ‘National ‘Maltina Dance All’ msimu wa nane (2014).

Video ya TONIGHT ilifanyika huko Port Harcourt nchini Nigeria na kuongozwa na muongozaji mwenye kipaji, Eddie iZcs wa EMPRESSIONISTO.

Kwenye TONIGHT,  Rave anaonesha mitindo ya kuvutia ya uchezaji unaofanya mashabiki waone upande wake mwingine: muziki wa kipekee utakaokushawishi kuinuka na kucheza. 

 Rave amepania kuleta uchezaji wake wa nguvu na muziki wake Afrika Mashariki. 

 Akitarajia kufanya ziara Afrika Mashariki,  Rave anasema, “ Ndoto yangu siku zote imekuwa kuwafikia na kuwahamasisha vijana, hivyo kitendo cha kuweza kuwafikia vijana wa Afrika Mashariki, kimevuka matarajio yangu ya awali. 

Ninachoweza kusema kwa sasa ni Asante Sana! Naahidi kuja na muziki mzuri, mpya na wa tofauti.

 Kupitia muziki wangu nataka kuonesha upande mwingine wa Afrika kuwa ni sawa kutoka nje ya boksi na kufanya kitu tofauti.”

ITAZAME  ‘TONIGHT’


Video ya kwenye simu: goo.gl/ffwZhp

Hulkshare: bit.ly/TonightRAVE

Wimbo wa TONIGHT na artwork yake vimeambatanishwa kwenye email hii. Kuwa huru kusambaza uwezavyo kwenye mitandao unayoitumia.


Mfollow @skytanzania kwenye Instagram au soma makala zake mbalimbali kupitia bongo5.com

Entertainment & Music Publicity 
+254 721 368 983


"Life shrinks or expands in proportion to one's courage." - Anais Nin (French-Cuban Author)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad