![]() |
|
Wakuu wa
mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameikubalia Sudan Kusini kuwa
mwanachama wa jumuiya hiyo ya kikanda.
Mkutano wa
kilele wa Jumuiya hiyo jijini Arusha leo ,
Jumatano (Machi 02,2016) umepitisha
pendekezo la Baraza la Mawaziri juu ya uwanachama wa Sudan Kusini na pia
hali ya usalama nchini Burundi.
Kikao hicho
kilichodumu kwa muda wa takribani masaa matano kimelikubalia taifa hilo changa
kabisa barani Afrika kuwa mwanachama wake wa sita, kuungana na Tanzania,
Rwanda, Burundi , Uganda na Kenya.
Rais Magufuli
ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao
hicho, amewaambia wajumbe wa mkutano huo wa kilele kwamba sasa "Sudan ya
Kusini ni mwanachama halali wa jumuiya" hiyo.
Mkutano huo
pia umezungumzia kwa kina masuala ya maendeleo ndani ya jumuiya ikiwemo mipango
ya kujengwa kwa viwanda vya nguo na bidhaa za ngozi ili kuondoa kabisa biashara
ya uagizaji wa nguo kuukuu, maarufu kama mitumba, katika nchi hizo katika miaka
michachache ijayo
Mkutano huo
pia umeshuhudia uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya kielektroniki itakayotumiwa
katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na mwongozo maalum wa kimaaadili katika
biashara kwenye nchi wanachama wa jumiya hiyo.
Akizungumzia
kuhusu maendeleo ya jumuiya hiyo, Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dk.
Richard Sezibera, amesema kuwa jumiya hiyo inasonga mbele kwani itifaki
mbalimbali zimepitishwa kuanzia ushirikiano katika soko la pamoja, ushuru wa
forodha na sasa wanaelekea kufikia hatua ya Afrika Mashariki kuwa na sarafu
moja itakayotumika katika nchi zote wanachama.
Amesema kuwa
tayari jitihada zinaendelea katika kuondoa vikwazo mbalimbali katika sekta za
mawasiliano, biashara na usafiri "ili kuwapa wananchi wa Afrika Mashariki
fursa ya kuufurahia na kufaidi muungano" huo.
Katika
mkutano huo, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hakuhudhuria na badala yake
alimtuma makamu wake wa pili, Joseph Butore, huku serikali ya Sudan Kusini
ikiwakilishwa pia na makamu wa pili wa rais, James Waniiga.
Na katika
hatua nyingine kikao hicho kimepitisha jina la Liberate Mfumukeko kutoka
Burundi kuwa katibu mkuu mpya wa jumuiya
hiyo kuanzia Aprili 01 mwaka huu,2016.
|
Wednesday, March 02, 2016
Home
HABARI
MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA EAC:-Sudani Kusini Yakubaliwa Kuwa Mwanachama Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA EAC:-Sudani Kusini Yakubaliwa Kuwa Mwanachama Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment