|
Mkuu wa
ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akifurahi jambo na
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi (aliyeipa mgongo kamera) wakati
wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua
Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa
mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo
endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach
Resort, Mkoani Tanga. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika,
Firmin Matoko. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kongamano la
pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia
ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa
la Sahara (GEBR) limefanyika mkoani Tanga.
Wenyeji wa
kongamano hilo walikuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na
Utamaduni (UNESCO) ofisi ya Dar es salaam.
Akifungua
kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kupitia shirika lake la
maendeleo na ushirikiano la kimataifa (KOICA)
kuongeza muda wa mkataba wa mradi wa GEBR ambao unafikia ukomo mwishoni
mwa mwaka huu.
Akizungumza
na washiriki mbalimbali wapatao 40 kutokana ndani na nje ya nchi zikiwemo Ghana
na Nigeria kutoka Afrika, alisema ombi hilo linatokana na ukweli kuwa walengwa
wamekuwa wakifaidika na mradi huo, kwa kuweza kubadilisha maisha yao na kuwa
bora zaidi.
Makamu wa
Rais alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na kutoweka kwa
uotoasili unaotoa fursa ya uoto wa mimea zaidi ya 10,000, jamii 6,000 ya
wadudu, jamii ipatayo 1000 ya ndege warukao.
Aidha Samia
katika hotuba yake alirejea msimamo wa serikali wa kutaka kuhifadhi mazingira,
pamoja na kuziweka rasmi chini ya uangalizi halali jumla ya hekta milioni 33.5 za misitu asili, huku akitanabaisha kuwa
serikali pia ina mapori ya akiba yapatayo 800 pamoja na misitu mingine.
Aliwakumbusha
washikadau pamoja na nchi wafadhili kwamba Tanzania inakabiliwa na ukuaji
mkubwa wa idadi ya watu wake wanaotegemea raslimali kwa matumizi yao ya kila
siku pamoja na mahitaji ya nishati.
“Tunaelewa
kwamba kuna shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zinazopelekea uharibifu
wa misitu na mazingira”, alisema Samia na kuongeza kwamba kuna kupokonyana kwa
ardhi na maji.
Katika
warsha hiyo wafaidika wakubwa katika mradi huo, ambao walitekeleza kwa vitendo
elimu iliyopatikana kutokana na mradi huo, walikabidhiwa vyeti ya ushiriki kwa
vitendo na kwa ufanisi mkubwa walioonyesha.
Washiriki
hao wengi walitoka katika miradi midogo midogo inayotekelezwa Amani, Muheza
ambayo ni pamoja na ufugaji nyuki,
samaki, vipepeo na uyoga.
|
|
Awali, Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza aliwataka wakazi wa Tanga na Tanzania kwa
ujumla kutumia vyema nafasi adhimu kwenye miradi ya maendeleo inayogharimiwa na
wafadhili na kuwasihi wawe makini kwani mafanikio yao huwa ni kivutio kwa
wafadhili kuweza kuendelea kutoa ufadhili kwa misaada.
Mradi wa
GEBR ambao uko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wake, unafadhiliwa na serikali ya Korea kupitia Shirika lake la
Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA).
Mradi huo wa
Unesco wa binadamu na bayosfia (MAB) unatekelezwa nchini Ghana, Nigeria na
Tanzania kwenye milima ya Usambara.
Katika
hotuba yake Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Firmin Matoko
alimpongeza Makamu wa rais kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu
katika utawala tangu historia ya kuundwa kwa Tanzania.
Alisema
amefurahishwa sana na wanawake kuchukua nafasi kwa kuwa Unesco wameweka
kipaumbele wanawake katika maendeleo.
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili
kwenye ukumbi wa mikutano hoteli ya Tanga Beach Resort akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko.
Akizungumzia
mradi wa GEBR alisema umelenga kutekelezwa katia msingi wa wazo la UNESCO la
binadamu na bayosfia.
Alisema
kwamba mradi huo umelenga kutumia elimu ya asili, elimu ya sayansi na utamaduni
ili kuboresha maisha ya biandamu huku wakihifadhi mazingira.
Aidha
alitaka kuwapo ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo na hifadhi
ya bayosfia kwa lengo la kuwezesha maendeleo endelevu.
Washiriki wa mradi huo pia walipata nafasi ya
kutembelea eneo la hifadhi ya Usambara mashariki.
Naye Balozi
wa Jamhuri ya Korea, Bw Geum-Young Song alisema kwamba wataendelea kushiriki
katika mradi huo ambao umejikita katika kuwezesha maendeleo endelevu huku
mazingira yakihifadhiwa.
Maimuna
Tarishi.
|
|
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la pili la
Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na
uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga
Beach Resort Mkoani Tanga.
Alisema ni
lengo la taifa lake la kuwezesha hifadhi endelevu kwa maendeleo endelevu.
Aidha
alitaka kuwepo na fikra za mradi kuwa endelevu baada ya wafadhili kuondoka.
Viongozi
waliohudhuria siku ya ufunguzi ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Bw. Firmin
Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mh. Geum -Young Song, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Unesco nchini
Tanzania, Zulmira Rodrigues, Wawakilishi wa KOICA nchini Ghana, Nigeria na
Tanzania; mwakilishi wa KOICA nchini Korea, Seoul; na kamati za MAB kutoka nchi zinazotekeleza
mradi huo.
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua
Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya
kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa
Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi
wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
|
|
Mkuu wa
Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Afrika, Firmin
Matoko kuhutubia kwenye kongamano hilo.
|
|
Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO, Irina Bokova wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa
mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo
endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach
Resort Mkoani Tanga.
|
|
Balozi wa
Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song
ambao ni wafadhili wa mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui
akisoma taarifa yake baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufungua Kongamano hilo la pili la
Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na
uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara.
Warsha hiyo imefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
|
|
Pichani juu na
chini washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu
unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda
Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika
ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort
Mkoani Tanga.
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi
cheti Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Uyoga (DMGA), Bi Judith Simon Muro,
kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa
kijani kwa kulinda bayoanui.
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi
cheti Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira asili Amani (Amani Forest Nature Reserve
- ANR), Bi. Mwanaidi Kijazi, kwa
kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani
kwa kulinda Bayoanui. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia Mkurugenzi Mkuu Msaidizi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh.
Geum-Young Song (wa pili kushoto) pamoja
na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi
ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar (wa kwanza kushoto).
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi
cheti Amiri Saidi Sheghembe wa mradi wa Vipepeo Amani kwa kutambua mchango na
ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui.
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan , akifurahi
jambo na Mkurugenzi wa Shirika la
Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar.
|
|
Mgeni rasmi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
katika picha ya pamoja na washiriki kutoka nje ya Tanzania wanaohudhuria Kongamano
la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama
njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa
Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
|
|
Mgeni rasmi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi
endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini,
kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara
linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
|
|
Mgeni rasmi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNESCO walioshiriki kwenye maandalizi
ya kongamano hilo.
|
|
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo
na Afisa Tathimini na Logistki wa UNESCO Ofisi ya Dar es Salaam, Rahma Islem
(kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
|
|
Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko (kushoto) akisalimiana na
mmoja wadau wa maendeleo Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song
.
|
|
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi katika picha
ya kumbukumbu na Mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye pia ni Katibu Klabu ya
Safe Space inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira, Lilian Tadei wa Shule ya
Sekondari Potwe, Muheza.
|
|
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi
(kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
|






No comments:
Post a Comment