PICHA/VIDEO:-Waziri wa Afya, Mh.Ummy Mwalimu apokea msaada wa fedha wa Mil 220, kwa matibabu ya Wagonjwa wa Moyo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 02, 2016

PICHA/VIDEO:-Waziri wa Afya, Mh.Ummy Mwalimu apokea msaada wa fedha wa Mil 220, kwa matibabu ya Wagonjwa wa Moyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania, Mh. Ummy Ally Mwalimu leo Machi 02.2016, amepokea msaada wa fedha kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa msaada huo, jumla ya watoto 101, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo kwa gharama za fedha hizo.
Fedha hizo zilizotolewa na Jumuiya ya Kihindu waishio Dar es Salaam ijulikanayo kama BAPS Charity, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa na upendo waliouonyesha kwa watanzania wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.

 
Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad