LIGI YA MABINGWA ULAYA:-Haikuwa mechi nyepesi…Bayern Munich yasonga robo fainali kwa jumla ya mabao 6-4. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 17, 2016

LIGI YA MABINGWA ULAYA:-Haikuwa mechi nyepesi…Bayern Munich yasonga robo fainali kwa jumla ya mabao 6-4.

Bayern Munich Pichani, ilipindua Matokeo ya 2 – 2 na kushinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Juventus katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Allianz Arena usiku wa Jumatano,March 16, 2016  na kusonga robo fainali  kwa jumla ya mabao 6-4.
Haikuwa mechi nyepesi, kwani hadi mapumziko walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 na mchezo huo ukaenda dakika 120, huku mabao ya Bayern Munich yakifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 73, Thomas Muller dakika ya 91, Thiago Alcantara dakika ya 108 na Kingsley Coman dakika ya 110.


Juventus magoli yao yalifungwa na Paul Pogba dakika ya 5’’ na Juan Cuadrado dakika ya 28 ya Mchezo huo.

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI.

-Real Madrid

-VfL Wolfsburg

-Paris St Germain

-Benfica

-Man City

-Atletico Madrid

- FC Barcelona

- Bayern Munich

Raundi ya Mtoano

-Droo ya Robo Fainali: Machi 18,2016.

**Mechi Aprili 05/06 na Marudiano Aprili 12/13,2016.

-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15,2016.

**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 03/04,2016.

FAINALI

Mei 28,2016.

San Siro, Milan, Italy

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad