|
Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala
Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa
ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni
Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.
|
|
Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala
Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha
Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho
kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la
ekari 500 la kupewa mwekezaji.
Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala
Mabula,amemsimamisha kazi Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na nyumba wa wilaya ya
Chato Mkoani Geita Bw Emmanuel Mogasa ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma
zinazomkabili
Uamuzi huo
ameutoa Juzi ,February 24,2016 katika
ziara ya Kikazi ya Siku 2 wilayani Chato Mkoani Geita ambapo alimtaka Msajili
wa Mabaraza ya Ardhi wa Kanda ,Bi Doroth Philip kupeleka haraka Mwenyekiti
mwingine wa Baraza la Ardhi wilayani humo ili wananchi waendelee kupata huduma
Amesema
Mwenyekiti huyo amekuwa akilalamikiwa na Wananchi kwa muda mrefu kutokana na
kukithiri kwa vitendo vya rushwa, kufanya kazi kwa mazoea, kuchelewesha maamuzi
ya kesi na kupindisha haki katika baadhi ya migogoro
Baadhi ya
wakazi wa Chato wameonekana kupokea uamuzi huo kwa hisia tofauti ambapo Bw
Mateso Misana amepongeza uamuzi huo huku Bw Cosmas Edward akisema kuwa Haki
haijatendeka kwa madai kuwa karibu Mabaraza yote nchini yamekuwa yakilalamikiwa
kwa kutotenda haki
Katika Ziara
hiyo Pia ,Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt
Angeline Sylvester Lubala Mabula ameagiza
Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi, Azitaka kulisaidia Shirika la
Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu sambamba na Halmashauri zinunue
nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao.
Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba
bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya.
|





No comments:
Post a Comment