![]() |
|
Asilimia 76
ya wananchi wanaamini kuwa utolewaji wa elimu bure utaongeza ubora wa elimu kwa
kuboresha mazingira ya kufundishia (asilimia 55).
Pamoja na
imani hiyo, asilimia 15 ya wananchi walisema elimu ya bure haitaboresha elimu,
kwa kuwa kuongezeka kwa uandikishwaji wa wanafunzi kutatumia rasilimali (fedha)
nyingi 8.
Asilimia 49
walisema wanafunzi hawatafanya vizuri kutokana na kukatazwa kwa masomo ya ziada
ambayo walimu waliyatumia kuwasaidia wanafunzi wasiofanya vizuri huku
wakijipatia kipato cha ziada. Pamoja na hayo asilimia 22 wana hofu na
upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia 9 .
Jambo la 2:
Asilimia 89 ya wazazi huchangia elimu ya umma.
Michango
imekuwa ni sehemu ya mfumo wa elimu baada ya upanuzi wa Elimu ya Msingi kwa
Wote. Asilimia 89 ya wazazi waliohojiwa walikiri kuchangia fedha kwenye shule
za umma.
Wazazi
walipoulizwa kuhusu kiwango cha fedha walichochangia, asilimia 80 walisema
wamechangia TZS 50,000 ama pungufu kwa mwaka, huku asilimia 8 wakichangia zaidi
ya TZS 100,000 .
|
![]() |
|
Michango inayotolewa
kwenye shule za umma hutumika kugharamia ulinzi (asilimia 66), majaribio
(asilimia 57) na madawati (asilimia 34). Kiwango kidogo hutumika kwenye
mahafali (asilimia 4) na safari za kishule (asilimia 4).
Utaratibu wa
ugawaji wa fedha za ruzuku ni: asilimia 40 vitabu na nyenzo nyingine za
kusomea; asilimia 20 kwa ajili ya vifaa vya kuandikia (kalamu, madaftari,
penseli n.k.); asilimia 10 kwa shughuli za kiutawala na asilimia 10 kwa ajili
ya makaratasi ya mitihani na uchapishaji.
Hivyo basi, maamuzi ya kuwa ruzuku
itumike vipi yanakuwa changamoto kwa upande wa shule zenyewe, na hata hivyo,
inaonekana wazi kuwa michango hulipia vitu vingi zaidi kuliko ruzuku.
|
![]() |
|
Jambo la 3:
Asilimia 49 ya wazazi wanaamini michango ya wazazi haitumiki ipasavyo.
Japokuwa
wazazi wengi wamekuwa wakitoa michango ya ziada, asilimia 49 ya wazazi
wanaamini kuwa fedha hizo hazitumiki ipasavyo. Wazazi wa mjini wana mashaka
zaidi ambapo asilimia 57 wanasema hivyo ukilinganisha na asilimia 44 ya wazazi
wa vijijini.
Vilevile
asilimia 58 ya wananchi wanaamini kuwa michango hii haijaidhinishwa na
serikali.
Asilimia 89 wanaamini kuwa walimu wa shule za umma huchangisha fedha
hizo kama chanzo cha kujipatia kipato cha ziada 11 .
|
![]() |
|
Jambo la 4:
Wananchi wanahusisha mafanikio ya ujifunzaji na juhudi za mwalimu.
Wananchi
walipoulizwa kuwa ni nini ambacho wanadhani kinachangia matokeo ya darasa la
saba kwenye jamii yao (kuwa mazuri ama mabaya), nusu yao walihusisha matokeo na
juhudi za mwalimu 12 .
Asilimia 7 pekee ndio waliotaja changamoto zinazohusiana
na wazazi au wanafunzi wenyewe 13 .
Cha
kushangaza ni kwamba mwananchi 1 kati ya 3 hajui nini kinachangia matokeo ya
kujifunza pindi watoto wanapohitimu elimu ya msingi.
|
![]() |
|
Jambo la 5:
Wananchi wanaamini kuwa walimu wanaona fahari juu ya taaluma yao lakini
hawapendi kazi yao.
Asilimia 93
ya wananchi wanaamini kuwa ualimu ni taaluma ambayo ndiyo msingi wa taifa.
Japokuwa asilimia 79 ya wananchi wanaamini kuwa walimu wanaona fahari ya kile
wanachokifanya, asilimia 80 wanaona kuwa walimu hawapendi kazi zao na hufanya
tu kwa ajili ya kujipatia kipato.
Je ni kwanini walimu wanaona fahari ya
taaluma yao lakini hawapendi kazi yao?
Kwa mujibu
wa baadhi ya wananchi, ni kutokana na mishahara pamoja na mazingira ya kufanyia
kazi.
Kwa ujumla asilimia 42 ya wananchi wanaamini kuwa walimu hawalipwi
vizuri, na asilimia 34 wanaamini mazingira ya kazi ya walimu hayawapi motisha
wa kufundisha.
Haya ni
maoni ya wananchi wachache (wananchi wengi wanatoa kauli zinazokinzana), lakini
yanaweza kutoa mwanga kwanini wananchi wanadhani walimu hawapendi kazi yao.
|
![]() |
|
Wananchi
walipoulizwa kuhusu vitu ambavyo vinaweza kuwaongezea walimu motisha ili kutoa
elimu bora kwa wanafunzi, asilimia 56 walisema nyongeza ya mishahara na
asilimia 19 walitaja uboreshaji wa mazingira ya kazi.
|
![]() |
|
Jambo la 6: Maoni ya wananchi
yanatofautiana juu ya ubora wa elimu ya msingi.
Wananchi
walipoulizwa kuhusu ubora wa elimu, nusu yao waliamini kuwa ubora wa elimu ya
msingi umezorota ama kubaki vilevile kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita,
huku nusu nyingine wakisema elimu ya msingi imeboreshwa.
|
![]() |
|
Wananchi
walio wengi wanaamini njia kuu ya kuboresha elimu ya msingi ni kwa kuweka mkazo
kwa walimu.
Ili kuboresha elimu wananchi wametoa ushauri ufuatao kwa serikali:
kufuatilia utendaji wa walimu (asilimia 40), kuongeza mishahara ya walimu
(asilimia 19), pamoja na kuongeza idadi ya walimu (asilimia 10). Asilimia 7
pekee ndiyo waliotaja ushirikiano kati ya mwalimu na
mzazi kama njia ya kuwawezesha watoto kujifunza.
|
![]() |
|
3. Hitimisho.
Serikali
mpya imejikita kwenye utoaji wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari na
wananchi wamekuwa na imani kubwa juu ya suala hilo. Wananchi wanaamini kuwa
utoaji wa elimu bure utatekelezwa katika muda ulianishwa, na ubora wa elimu
utaongezeka.
Wasiwasi wa
wananchi unaonekana kwenye uwajibikaji wa walimu katika kufikia kiwango cha juu
cha elimu. Walipoulizwa kuhusu namna ya kuboresha elimu ya msingi, wananchi
walitilia mkazo kwenye mishahara ya walimu, kuongezeka kwa idadi ya walimu
mashuleni na zaidi ya yote uwajibikaji
wa walimu.
Siyo
wananchi pekee wanaosisitiza uwajibikaji wa walimu. Kwa mujibu wa Davidson,
ukosefu wa motisha kwa walimu ni moja ya sababu kuu inayoathiri ubora wa elimu
nchini Tanzania 16 .
Utafiti usio
rasmi uliofanywa na Twaweza kwa walimu 272 unaonesha kuwa asilimia 96 ya walimu
hao hawaridhishwi na kazi zao.
Pia, mwalimu
1 kati ya walimu watatu alisema asingechagua tena kazi ya ualimu, huku wakitaja
mazingira magumu ya kazi (asilimia 34) na mishahara midogo (asilimia 26) kama
sababu kuu. Hii inadhihirisha kuwa walimu na wananchi kwa ujumla wana mitazamo
inayofanana.
Kwa kuwa
uongozi mpya umeweka mkazo suala la elimu, ni vizuri pia ukaanza kutatua
matatizo ya walimu na kuboresha mazingira ya ufundishaji Tanzania ili kwenda
sambamba na kasi ya utoaji wa elimu.
Wakati
utekelezaji wa sera mpya ya Elimu ukiendelea, ni vyema kufuatilia mabadiliko
yaliyofanyika na mafanikio yaliyopatikana.
Kumekuwa na
kusitasita kuhusu dhana hii ya ‘elimu bure’ ambapo viongozi wa shule wana
mashaka na jinsi ambavyo TZS 10,000 kwa kila mwanafunzi mmoja kwa mwaka inaweza
kutosha. Mfano mmoja ni kuhusu suala la ulinzi.
Kama
ilivyoelezwa hapo juu, asilimia kubwa ya michango ya wazazi kwa mwaka 2015
imekuwa ikitumika kwenye ulinzi (asilimia 66); wakati ruzuku inayotumwa shuleni
haihusishi suala la ulinzi.
Iwapo fedha
zote zilizotengwa zitapelekwa shuleni na kuwafikia wahusika kwa kiwango
kilichopangwa, je kiwango hicho kitatosha kuhakikisha watoto wanajifunza?
Suala
jingine la msingi ni kuhusu utunzwaji wa rasilimali. Ruzuku hapo awali zilikuwa
zinapelekwa moja kwa moja shuleni mpaka mwaka kufikia mwaka 2002 zilipoanza
kupelekwa kupitia kwa mamlaka zaHalmashauri za Wilaya na Miji.
Kwa sasa
mfumo umebadilika ambapo ruzuku zinapelekwa moja kwa moja shuleni. Tunaamini
uamuzi wa kupeleka ruzuku moja kwa moja mashuleniumechangiwa na na kutokuwepo
kwa ufanisi katika mfumo uliopita.
Kwa mfano,
kati ya 2010 na 2013, kwa wastani ni TZS 2,202 pekee ndizo zilizofika shuleni
kwa kila mwanafunzi.
Sera mpya ya
kupeleka pesa za ruzuku moja kwa moja mashuleni unaibua maswali kadhaa.
Tutahakikisha vipi upelekaji wa pesa moja kwa moja kwenye shule utatupa matokeo
tofauti?
Je shule
zina uwezo wa kusimamia rasilimali hizo vizuri; kuzuia ubadhirifu na upotevu na
kuhakikisha zinaelekezwa kwenye matumizi ya vitu muhimu zaidi? Kuna mfumo gani
uliopo kwenye ngazi ya shule, hususani katika kuhakiki maamuzi ya matumizi?
Ili
kuhakikisha tunapata thamani halisi ya matumizi katika elimu, utoaji na
matumizi ya fedha vinapaswa kuhakikiwa katika ngazi ya shule.
Kwa
kumalizia, na la muhimu zaidi, utawala mpya umeonekana kuwa kimya kwenye suala
la kuboresha matokeo ya ujifunzaji. Ongezeko la shule za msingi kwa mamilioni
ya watoto wa kitanzania ni mafanikio makubwa.
Hata hivyo,
baada ya miaka kumi ya sera hii, tunatilia shaka anguko la uandikishaji huo wa
maelfu ya watoto pasipo kutoa fedha za kutosha, wala kutilia mkazo suala la
ubora. Je kutakuwa na walimu wa kutosha kwa wanafunzi hawa? Tutahakiki vipi
kama wanajifunza?
Kwa kipindi
cha miaka kumi iliyopita tumeshuhudia ongezeko kubwa la shule za sekondari
pamoja na wanafunzi huku ikiambatana na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi
wanaofanya vibaya kwenye mitihani yao ya kidato cha nne.
Je uongozi
huu umejipanga kufanya nini cha tofauti kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei
kutengeneza wahitimu mbumbumbu?
Tutahakikisha
vipi mfumo wa elimu unawapa watanzania fursa ya kuishi maisha mazuri na
kuchochea maendeleo ya nchi? Pamoja na nia njema na maelezo mazuri ya Rais
yanayotilia mkazo kwenye elimu na kutoa matumaini mapya, ni muhimu kuzingatia
kuwa ufanisi katika sekta hii muhimu utafikiwa kwa kutumia ushirikiano na wadau
wote.
Aidha,
panahitaji marekebisho mapana zaidi katika mfumo wa elimu ili kufikia malengo
ya elimu bure na bora, na sio bora elimu bure!
|















No comments:
Post a Comment