Mwanamuziki
mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya
Kundi zima la Mjomba Band.
MWANAMUZIKI
mkongwe wa muziki Dansi Nchini Tanzania, Kassim Mapili amefariki dunia akiwa chumbani kwake,
Tabata jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi
(CHAMUDATA) Hassan Msumari, amesema kuwa kifo cha Mapili kimegunduliwa usiku wa Jana February 25,2016 baada ya mlango wa chumba chake kuvunjwa.
Mlango huo
ulivunjwa baada ya Kassim Mapili kutoonekana tangu alipokwenda kutazama mpira
wa Arsenal na Barcelona Jumanne,February 23,2016, usiku.
Kwa mujibu
wa Msumari, mara mlango ulipovunjwa Kassim Mapili alionekana akiwa ameshafariki
akiwa amejifunga taulo, ishara inayoonyesha kuwa aidha alikuwa anakwenda kukoga
au ametoka kukoga.
Jumatatu
jioni Kassim Mapili alishiriki vizuri mazishi ya mwanahabari Fred Mosha
makaburi ya Kinondoni ambapo alipewa wasaa wa kuongea machache na kama vile
hiyo haitoshi, Mapili aliimba makaburini hapo kuomboleza kifo cha Fred Mosha.
(CREDIT:
SAID MDOE)
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630Or+255756830214.
No comments:
Post a Comment