|
Mwezeshaji
katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake,
vijana na watu wenyeulemavu, Bi.Valeria Msoka akizungumza katika warsha hiyo.
|
|
Mwezeshaji
katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea
wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka (kulia) akizungumza katika
warsha hiyo.
|
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (kulia) akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya
habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu,
ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini
Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA.
|
|
Bi. Stella
Jairos ambaye ni miongoni mwa wagombea walioshiriki Uchaguzi Mkuu 2015
wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha hiyo. Bi. Jairos aligombea
Ubunge Vitimaalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi
Wetu
CHAMA cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea
nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha
kuzungumza kwenye vyombo vya habari.
Alisema utafiti mdogo walioufanya katika
vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea
ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo.
Takwimu hizo
zilitolewa jana katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya
wagombea na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA,Bi Edda Sanga alipokuwa akifungua semina
hiyo ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini
Tanzania.
Alisema
katika utafiti huo uliofanywa kwa miezi miwili yaani Septemba na Oktoba 2016
kwenye magazeti sita ulibaini kati ya vyanzo vya habari 2577 vilivyotumika
kwenye habari za Uchaguzi Mkuu, wanaume waliotumika kama vyanzo walikuwa 2256
ikiwa ni sawa na asilimia 88 huku wanawake 303 kama vyanzo hii ikiwa ni
asilimia 11 tu.
Mkurugenzi
huyo Mtendaji wa TAMWA alisema utafiti pia uliainisha kuwa wanaume waliongoza
katika makundi yote ya mada za habari hata zile ambazo hazikuwa zikihusiana na
uchaguzi huo.
Aliongeza kuwa katika utafiti huo ilikuwa ni nadra sana kupata
habari ambazo zipo katika kurasa za mbele huku vyanzo vyake vikiwa vimetokana
na wanawake. Habari za wanawake zilianza kujitokeza kuanzia kurasa za nne na
kuendelea.
"...Kwa
mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji wa habari za magazeti, wanawake kwa ujumla
waliogombea na wasiogombea kote nchini walikabiliwa na unyanyasaji kama vile
kufanyiwa ghasia, na vitisho wakati wa kampeni na siku ya uchaguzi.
Pia wanaume
walificha kadi za kupigia kura za wanawake zao, wanaume waliwalazimisha wake
zao kuwapigia kura wagombea ambao wanawataka hata kama mwanamke hamtaki,
utumiaji wa lugha ya matusi dhidi ya wagombea wanawake na wakati wa kampeni
kuna baadhi ya wagombea wanawake walikamatwa na kutishiwa kwa tuhuma za kutotii
amri ya Jeshi la Polisi," alisema Sanga katika taarifa yake akifungua
semina hiyo.
|
|
Baadhi ya
wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea
changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari
pamoja na wagombea hao.
|
|
Baadhi ya
wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea
changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari
pamoja na wagombea hao.
|
|
Baadhi ya
washiriki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na
baadhi ya wagombea walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu 2015 kuzungumzia
changamoto za kutopewa nafasi wagombea wanawake, vijana na walemavu kwenye
vyombo vya habari.
Kwa upande
wao wanawake waliogombea wakizungumza katika semina hiyo walisema vyombo vya
habari kiujumla havikutoa nafasi sawa kwa wagombea hasa wanawake na vingi
vilikimbilia kutoa habari za wagombea wenye majina na maarufu kwa wanajamii.
Bi. Stella Jairos ambaye aligombea Ubunge Vitimaalum Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Dodoma alisema wanawake walemavu mbali na kukosa fursa kwenye vyombo vya habari
walikabiliwa na changamoto mbalimbali zilizofifisha mafanikio katika
kinyang'anyiro cha uchaguzi huo.
Naye, Loyce
Kibona aliyegombea upande wa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo alisema
licha ya vyombo vya habari kuwa ni changamoto kwao kupata nafasi ya kusikika
bado hali ya kujiamini kwa wanawake na kukatishana tamaa kunaendelewa
kukwamisha mafanikio ya kundi hilo hivyo kuwataka wanawake kuungana mkono.
Imeandaliwa:
www.thehabari.com.
|





No comments:
Post a Comment