|
Wakili wa
kafulila profesa safari akiongea na waandishi nje ya mahakama ya hakimu
mfawidhi wa mkoa baada ya jaji kuhairisha kesi.
Na Editha
Karlo wa blog ya jamii Kigoma
KESI No. 2
ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma kusini
iliyofunguliwa na mlalamikaji David
Kafulila dhidi ya mbunge Hasna Mwilima,Msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria
mkuu wa serikali imeahirishwa leo na mahakama kuu kanda ya Tabora mpaka marchi 9, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa
tena.
Kesi hiyo
ambayo ilikuwa ianze mapema leo katika
mahakama ya hakimu mkazi Kigoma, Mbele
ya Jaji Dr Wambari ambae pia ni Mkuu wa chuo cha sheria lushoto mkoani Tanga,
imeahirishwa kwasababu mshatakiwa Hasna pamoja na wakili wake Kennedy
Fungamtama pamoja na mawikili wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo, kwa
madai ya kuchelewa kupata wito wa mahakama hyo, huku mlalamikaji David Kafulila
akifika na wakili wake Prof Safari.
Katika
mazingira hayo Jaji Wambari aliagiza mawasiliano yafanyike kwa pande hizo ili
kujua ni lini kwa hakika mawakili hao wataweza kushiriki katika kesi hiyo.
Kutokufika
kwa mlalamikiwa na mawakili wake na wale
wa upande wa serikali ilipelekea zoezi la kusikiliza kesi hiyo kusimama kwa saa
mbili kutoka saa tano asubuhi mpaka saa
saba mchana na baada ya hapo hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya
Jaji silivesta Kahinda alisema kuwa kesi
itaendelea march 9 mwaka huu na kwamba kwakuwa tarehe hiyo imependekezwa na
mawakili na pande zote mbili.
Akiongea na
mtandao huu mlalamikaji wa kesi hiyo David Kafulila alusema luwa anakubiana na
uamuzi wa mahakama hivyo aliwataka wananchi wawe na subiri hadi hiyi tarehe 9
march mwaka huu.
""Jaji
mkuu na Jaji kiongozi wamekuwa dhamira
kwa sasa kuwa kesi za uchaguzi zimalizike haraka na hivyo kufikia tarehe
hiyo ya march 9,2016 kesi inatarajiwa
kusikilizwa mfululizo .
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment