Kampuni ya
Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia
kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni
Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa
washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya
StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa
Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya
B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
|
Baadhi ya
Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya
Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na
washindi.
|
Alexander
Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION lililoandaa mashindano hayo akizungumza
wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza
kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa
ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha
ujenzi wa jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi
Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.
|
Fredy Samwel
Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika
Mashindano hayo.
|
Alfredy
Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati
wa mashindano hayo.
|
Mwenye
kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa
tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano hayo.
Amesema
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE
FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto
zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.
|
Dickson
Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya
akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi
nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.
|
Msanii
Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa
Jijini Mwanza.
|
Majaji
ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji
Lilian Lambo
|
Wa pili
kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS
pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo.. Imeandaliwa
na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP.
|
No comments:
Post a Comment