![]() |
|
Askari
polisi watatu wamefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya gari lao
lililokuwa kwenye msafara wa Rais John Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma,
kupasuka tairi na kupinduka.
Rais Magufuli
alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya
kuzaliwa kwa CCM.
Hiyo ni mara
ya pili kwa askari kufariki wakiwa kwenye msafara wa Dk Magufuli baada ya
aliyekuwa akiongoza msafara wake wakati wa kampeni kugongana na dereva bodaboda
katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari huyo
alikuwa kwenye pikipiki maalumu iliyokuwa ikiongoza msafara wakati Dk Magufuli
akitoka katika Hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,
Deo Filikunjombe.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo ilitokea Jana February 06,2016, saa
9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi mkoani humo baada ya
moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva kushindwa kulimudu.
|


![]() |
|
Aliwataja
waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.
Waliojeruhiwa
ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Singida (RCO), Peter Majira (50,na PC
Charles Simon (34) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Gari hilo
lililopata ajali ni lile lililokuwa limetangulia ili kufagia barabara kabla ya
msafara wa Rais, likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha
mkoa huo.
Sedoyeka
alisema miili ya askari hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali
ya mkoa huo.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Kitundu Jacks alisema hali za
majeruhi waliofikishwa kwenye hospitali hiyo zinaendelea vizuri.
“Mrope ndiye
aliyeletwa akiwa kwenye hali mbaya, alikuwa amevunjika mbavu na mkono na akafa
mara tu baada ya kufikishwa hospitalini hapa. Majeruhi wengine wamepata
michubuko na wanaendelea vizuri,” alisema.
|


![]() |








No comments:
Post a Comment