|
Watu sita
wanaodaiwa kuwa majangili, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuitungua
helikopta ya doria na kusababisha kifo cha rubani wake katika pori la akiba la
Maswa.
Kukamatwa
kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais, John Magufuli, kutoa agizo kwa
Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamatwa waliohusika na tukio hilo na
kufikishwa katika mkono ya sheria.
Kauli hiyo
ya Rais iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson
Msigwa, ilisema Rais Magufuli mbali na
kusikitishwa na tukio hilo, pia aliuakikisha umma kuwa serikali itahakikisha
inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zote na kuwataka wananchi na
wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori kutokatishwa tama.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy, jana February 01,2016 alithibitisha kukamatwa kwa watu hao.
Alisema
awali walikamata watu wawili, juzi watatu na jana mmoja wote wakiwa wakazi wa
Simiyu na uchunguzi bado unaendelea.
Ijumaa
iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo wakati ikifanya doria katika pori hilo baada
ya kuwapo taarifa kwamba majangili walikuwa wameua tembo mmoja.
Katika tukio
hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower (37) alikufa,
huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment