|
Jana
February 24,2016, Manchester imejiweka
vyema kutinga Robo Fainali baada ya kupata ushindi mnono Ugenini katika Mechi
ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI 2015/2016
walipoichapa Dynamo Kiev Bao 3-1 huko Kiev, Nchini Ukraine.
Man City,
ambao walibadili Wachezaji 10 toka kile Kikosi kilichodundwa 5-1 na Chelsea
kwenye FA CUP Jumapili iliyopita, walitawala Kipindi cha Kwanza na kupiga Bao 2
kupitia Sergio Aguero na David Silva zilizofungwa Dakika za 15 na 40.
Vitaliy
Buyalsky aliipa Bao Dynamo katika Dakika ya 58 na Gemu kuwa 2-1 lakini Yaya
Toure akawakata maini katika Dakika ya 90 kwa Shuti murua la kupinda na kufunga
Bao la 3 na kuwapa City ushindi mnono wa 3-1 kuelekea Mechi yao ya Marudiano
hapo Machi 15 Uwanjani Etihad.
Katika Mechi
nyingine ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL PSV Eindhoven na
Atletico Madrid zilitoka Sare 0-0 huko Mjini Eindhoven Nchini Uholanzi.
PSV walibaki
Mtu 10 kuanzia Dakika ya 58 baada ya Pereiro kupewa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi
za Njano 2.
UEFA
CHAMPIONZ LIGI 2015/2016 -RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
JUMANNE 08 MAR 2016
Real Madrid
v AS Roma [2-0]
VfL
Wolfsburg v KAA Gent [3-2]
JUMATANO 09 MAR 2016
2000 Zenit
St Petersburg v Benfica [0-1]
Chelsea v
Paris St Germaine [1-2]
JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico
Madrid v PSV Eindhoven [0-0]
Man City v
Dynamo Kiev [3-1]
JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v
Arsenal [2-0]
Bayern
Munich v Juventus [2-2]
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment