Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu msimu
ujao 2016/2017 kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na vyombo husika vya TFF
baada ya michezo ya kundi hilo kuchezwa leo,February 13,2016 jioni katika
viwanja tofauti nchini.
TFF imefikia
hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa
v Geita Gold na Polisi Tabora v JKT Oljoro iliyochezwa leo jioni katika mikoa
ya Kigoma na Tabora.
Taarifa za
michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili
zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF.
Katika
michezo hiyo ya leo, Geita iliibuka na ushindi wa mbao 8 – 0 dhidi ya JKT
Kanembwa, huku Polisi Tabora wakiibuka na ushindi wa mabao 7 – 0 dhidi ya JKT
Oljoro.
IMETOLEWA NA
TFF
Matokeo.
Jumamosi Februari 13,2016.
Kundi B
Kimondo
FC 2 - 0 Kurugenzi FC
Njombe Mji 2
- 0 Lipuli FC
Ruvu
Shooting 0 – 0 Polisi Morogoro
Burkinafaso
FC 2- 3 JKT Mlale
Kundi C
Mbao FC 1 –
1 Polisi Mara
Polisi
Tabora 7 – 0 JKT Oljoro
JKT Kanembwa
0 – 8 Geita Gold FC
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment