Tukio hilo
lilitokea Februari 09, saa 2.42 usiku, baada ya watu watatu kufika dukani kwake,
mmoja wao akiwa na bunduki kisha kumwamuru atoe fedha alizokuwa nazo.
Manguye
alisema alichukua Sh80,000 alizokuwa nazo na kumkabidhi jambazi huyo, lakini
hakuridhika na kumlazimisha aongeze kiasi kingine.
“Nilipandwa
hasira nikanyanyuka wakati jambazi anainama kuangalia kwenye kiboksi cha fedha,
nikamkamata kifuani na kung’ang’ania mkanda wa bunduki, akaanza kunivuta kwenda
nje, nami nikamvutia ndani, lakini alifanikiwa kunitoa nje akaniangusha chini,
lakini sikuachia mkanda wa bunduki,” alisema Manguye na kuongeza:
“Aliposikia
wananchi wameanza kupiga yowe akaniachia na kutoa mkanda wa silaha begani,
akakimbia na kuniachia bunduki. Wakati huo huo jambazi mwingine alikuwa
amekamatwa kwenye duka la Zaituni Magasi, wananchi walipofika wakaanza
kumshambulia, wakati huo taarifa ilikuwa tayari imetolewa Kituo cha Polisi
Sirari, wakafika kumchukua,” alisema.
|
Hii ni mara
ya pili kwa Manguya kuvamiwa na majambazi wenye silaha, ambapo mwaka 2014
alivamiwa dukani kwake na majambazi waliokuwa na bunduki, lakini alifanikiwa
kumpiga kwa kigoda aliyekuwa na bunduki na alianguka chini.
Magasi
alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa amevamiwa na majambazi waliokuwa na
bunduki, mapanga na nondo.
“Wakati
anatoka mvunguni mdogo wangu alimkamata kwa nyuma na kummudu huku akipiga
kelele, watu wakafika wakaanza kumpiga hadi akazimia, polisi walipofika
wakamwokoa kwani kidogo wamuue,” alisema.
|
No comments:
Post a Comment