CAF CHAMPIONZ LIGI 2015/2016:-Yanga SC yashinda 1 – 0 dhidi ya Cercle de Joachim. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 13, 2016

CAF CHAMPIONZ LIGI 2015/2016:-Yanga SC yashinda 1 – 0 dhidi ya Cercle de Joachim.

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, Leo,February 13,2016 wameanza Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Cercle de Joachim ya Visiwa vya Mauritius kwa ushindi wa Bao 1-0.

Bao hili muhimu la Ugenini la Yanga lilifungwa na Straika Donald Ngoma katika Dakika ya 17.

Mara baada ya Mechi yao hiyo ya Mauritius, Yanga watarejea Nyumbani na kupiga Kambi huko Visiwani Pemba ili kujifua kwa ajili ya Mechi yao ya Februari 20, ile Dabi ya Kariakoo, dhidi ya Mahasimu wao Simba ikiwa ni Mechi ya Ligi Kuu Vodacom.

Yanga SC watarudiana na Cercle de Joachim hapo Tarehe 20 Februari Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad