TASWIRA PICHA:-Zaidi ya Magari 400 yakwama eneo la Nyabugombe-Mkoani Kagera baada ya barabara Kuharibika. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 27, 2016

TASWIRA PICHA:-Zaidi ya Magari 400 yakwama eneo la Nyabugombe-Mkoani Kagera baada ya barabara Kuharibika.


Pichani ni eneo hilo la Nyabugombe na ni  magari yakiwa kwenye msururu huku wasafiri wakiwa na mizigo kichwani kutafuta namna mbadala ya kujikwamua katika eneo hilo.



Zaidi ya magari 400 ya mizigo na abiria wanaosafiri kutoka Jijijini Dar es salaam na Mikoa mingine kuelekea Nchi za Burundi na Rwanda wamekwama kwa zaidi ya siku nzima katika barabara ya Nyakanazi – Benaco katika eneo la Nyabugombe wilayani Biharamulo mkoani Kagera kutokana na ubovu wa barabara hali iliwasababishia usumbufu mkubwa na gharama.

Hata hivyo hali imekuwa ngumu zaidi kwa wasafiri ambao wakizungumza bila matumaini wameelezea mazingira magumu yanayowakabili katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kukosa huduma za msingi kama chakula na mawasiliano ya simu kutokana na eneo hilo kukosa network.

Wakizungumza,Madereva  waliokwama hapo wamesema kuwa kukwama kwao ni kutokana na ubovu wa barabara pamoja na matengezo ya awali yaliyofanyika ambayo  wamesema kuwa yapo chini ya kiwango na hasa mvua zinaponyesha.

Eneo hilo la Nyabugombe kwa muda mrefu limekuwa korofi kutokana na kukosekana kwa matengenezo ya uhakika katika barabara hiyo muhimu kibiashara kati ya nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.PICHA ZOTE NA SHABAN NDYAMUKAMA-NGARA.

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad