KLABU BINGWA AFRICA:- Yanga SC yaiondoa Mashindanoni Cercle de Joachim ya Mauritius kwa mabao 3-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 27, 2016

KLABU BINGWA AFRICA:- Yanga SC yaiondoa Mashindanoni Cercle de Joachim ya Mauritius kwa mabao 3-0.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara, Yanga SC leo,February 27,2016 imeifunga timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius mabao 2-0 na kuiondoa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-0.

Mechi hiyo imepigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga SC ilipata bao la kwanza dakika ya tatu tu ya mchezo kupitia kwa Amissi Tambwe huku Kipindi cha pili dakika ya 55, Thaban Kamusoko ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo aliifungia Yanga bao la pili kwa shuti kali akimalizia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa kwa mtindo wa pasi.

Katika hatua inayofuata Yanga SC itakabiliana na kati ya Mbabane Swallows au APR ya Rwanda.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad