Daniel Yona
akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili Hospitali ya Palestina, Sinza – Dar
es Salaam leo Jumatatu,February 08,2016.
|
Yona na
Mramba wakiwa wameshika vifaa vya
kufanyia usafi.
|
Wakioneshwa
mazingira ambayo watakuwa wakiyafanyia usafi kwa kipindi chote cha adhabu.
Ofisa
Mazingira wa Hospitali ya Palestina-Sinza, Bi. Miriam Mongi (mwenye brauzi
nyekundu) akimkabidhi Yona vifaa vya kufanyia usafi.
Yona na
Mramba wakiwa wamevaa ‘ovaroli’.
Ofisa Huduma
za Jamii wa Hospitali ya Palestina – Sinza, Bw. Deogratius Shirima akizungumza
na wanahabari hospitalini hapo.
Maeneo ya
hospitalini hapo.
.
Takataka katika baadhi ya maeneo hospitalini hapo.
Wanahabari
wakichukua matukio.
Waliokuwa
Mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ,leo Jumatatu,February 08,2016 wameanza kutumikia adhabu ya
kifungo cha nje, kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali
ya Sinza, Palestina, ya jijini Dar, kulingana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita kuhusu kesi iliyokuwa ikiwakabili.
Mramba
aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini
waliwasili mapema leo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Hospitali ya Sinza
Palestina ili kuanza kutumikia adhabu hiyo kama mahakama ilivyowaamuru.
Baada ya
kuwasili hospitalini hapo, Yona na Mramba walipokelewa na ofisa huduma za jamii
Bw. Deogratius Shirima na Wananchi wengine waliokuwepo kushuhudia vigogo hao
wakitumikia adhabu hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari hospitalini hapo, Shirima alisema kuwa, leo ilikuwa ni
siku ya kuwapa maelekezo namna ambavyo watafanya usafi, maeneo ya kufanya usafi
pia walikabidhiwa vifaa watakavyovitumia kufanyia usafi kuanzia kesho.
Baadaye
Afisa Mazingira hospitalini hapo Bi. Miriam Mongi, aliwakabidhi Yona na Mramba
vifaa vya kufanyia usafi ambavyo ni; mifagio, mafyekeo, viatu vya kufanyia
usafi maarufu kama “gambuti” na glovusi.
Oktoba 2,
2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi
ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia,
alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa
matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho
mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka
miwili na si miaka mitatu.
Mawaziri hao
wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu
namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili
wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya ndipo hivi karibuni baada
ya mahakama kupitia upya kesi hiyo ikaamuru wapewe adhabu ya kifungo cha nje
huku wakifanya kazi za kijamii kwa muda wa saa nne kila siku kwa miezi sita.
Na Denis
Mtima/GPL.
|
No comments:
Post a Comment