Wanafunzi
watatu wa shule ya Sekondari Kanazi wilayani Ngara Mkoani Kagera wamefariki
huku wengine 19 wakijeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa shuleni.
Mganga wa Zamu
katika Hospitali ya Murugwanza, walikokimbizwa Majeruhi hao Dr Edwin Ngeze
amesema wanafunzi hao watatu wamefariki muda mfupi baada ya kufikishwa kwenye
Hospitali hiyo kutibiwa majeraha na kwamba kati ya waliofariki ,Wasichana ni
wawili na Mvulana mmoja.
Imeelezwa
kuwa tukio hilo limetokea Jana ,February 10,2016, majira ya Saa Nane mchana
muda mfupi baada ya Wanafunzi hao kutoka kwenye viwanja vya michezo na
kukimbilia madarasani kwa ajili ya kujikinga Mvua ambapo ghafla ilipiga radi na
kuwajeruhi.
Dr Ngeze
amesema wanaendelea kuwahudumia majeruhi hao na kwamba taarifa rasmi itatolewa
baada ya uchunguzi kufanyika katika miili yao.
Akizungumza
katika Hospitali ya Murugwanza walikolazwa Majeruhi hao na kuhifadhiwa Miili ya
waliofariki, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Ngara, Bi
Honoratha Chitanda amesema Serikali itawagharamia matibabu waliojeruhiwa na
kushiriki maziko ya waliofariki.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment