Prof.Makame Mbarawa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ,Jana February 10,2016,jijini Dar es Salaam ,Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na
wafanyakazi wa shirika hilo.
“Kufuatia
upotevu huo Serikali imechukua hatua
thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi
ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi
cha polisi kitengo cha usalama
mtandaoni ili kubaini mtandao mzima
uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.
Vilevile
aliongeza kuwa Serikali imemuagiza
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi
kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa
tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.
Prof.Mbarawa
ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa
njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana
inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa
sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment