MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF:-Leo; Februari 28, 2016...Simba SC Vs Singida United ( Taifa).Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza) - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 28, 2016

MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF:-Leo; Februari 28, 2016...Simba SC Vs Singida United ( Taifa).Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)

Wakongwe; Nyota watatu wazoefu wa Simba SC, kutoka kulia Justice Majabvi, Awadh Juma na Mussa Mgosi wanatarajiwa kuibeba timu yao leo mbele ya Singida United.

Mashindano ya Kombe ka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation inatarajiwa kuendelea leo,February 28,2016 kwa michezo miwili ya hatua ya 16 Bora.

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabingwa wa mwaka 2000 wa Kombe hilo, Simba SC watakuwa wenyeji wa Singida United ya Singida, wakati Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wenyeji Toto African wataikaribisha Geita Gold ya Geita.

Singida inachagizwa na mafanikio ya kupandea Daraja la Kwanza kutoka la Pili wiki iliyopita, wakati Simba SC ina hasira ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa mahasimu, Yanga SC wiki iliyopita.

Mechi za 16 Bora ya michuano hiyo, zitahitimishwa kesho kwa mchezo mmoja, kati ya wenyeji Panone FC dhidi ya Azam FC ya Dar es Salaam Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Timu zilizotinga Robo Fainali za michuano hiyo hadi sasa ni nne, ambazo ni Yanga SC iliyoitoa JKT Mlale kwa kuifunga 2-1 Februari 24,2016, Ndanda FC iliyowatoa waliokuwa wanashikilia taji, JKT Ruvu kwa kuwafunga 3-0, Coastal Union iliyoifunga 1-0 Mtibwa Sugar juzi, Prisons iliyowafunga 2-1 Mbeya City na Mwadui FC iliyowafunga 3-1 Rhino Rangers.

MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF

Februari 24, 2016.

Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)

Februari 26, 2016.

Ndanda FC 3-0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 

Coastal Union 1-0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)

Februari 27, 2016.

Mwadui FC 3-1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) 

Prisons 2-1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)

Leo; Februari 28, 2016.

Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam) 

Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)

Kesho; Februari 29, 2016.

Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad