EPL 2015/2016:-Ushindi wa lala salama kwa Leicester City na Chelsea Mechi Ligi kuu Jana February 27,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 28, 2016

EPL 2015/2016:-Ushindi wa lala salama kwa Leicester City na Chelsea Mechi Ligi kuu Jana February 27,2016.

Goli  pekee la Leonardo Ulloa dakika ya 89, limeipa Leicester City (Pichani) ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich City Uwanja wa King Power katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza 2015/2016,hapo jana February 27,2016, jioni.

Ushindi huo unaifanya Leicester City izidi kukwea kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 27, ikiwazidi kwa pointi tano wote, Tottenham Hotspur Pointi 51 na Arsenal wanaofuatia kwa pia Pointi 51, wakiwa wamecheza mechi 26.

Spurs leo,Jumapili wanaikaribisha Swansea City Uwanja wa White Hart Lane, wakati Arsenal wanaifuata Manchester United Uwanja wa Old Trafford.
Branislav Ivanovic (kushoto) akienda juu zaidi ya Virgil van Dijk kuifungia Chelsea bao la ushindi kwa kichwa dakika ya 89 ,Hapo Jana February 27,2016.
Nao Chelsea walitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Southampton Uwanja wa St. Mary's, mabao yake yakifungwa na Cesc Fabregas dakika ya 75 na Branislav Ivanovic dakika ya 89, baada ya wenyeji kutangulia kwa bao la Shane Long dakika ya 42.

Leo Februari 27, 2016 .
 
West Bromwich Albion 3-2 Crystal Palace

Leicester City 1-0 Norwich City

Stoke City 2-1 Aston Villa

Watford 0-0 Bournemouth

Southampton 1 - 2 Chelsea

West Ham United 1-0 Sunderland

Kesho; Februari 28, 2016.

Tottenham Hotspur Vs Swansea City (White Hart Lane, Saa 11:05 jioni) 

Manchester United Vs Arsenal (Old Trafford, Saa 11:05 jioni)

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad