KOMBE LA TFF:- Azam FC hiyo kwa Yanga na Simba Nane Bora ya Kombe la Azam Sports Federation 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 29, 2016

KOMBE LA TFF:- Azam FC hiyo kwa Yanga na Simba Nane Bora ya Kombe la Azam Sports Federation 2016.


Wana lambalamba’’Azam FC’’ imekamilisha idadi ya timu nane za kucheza hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Panone FC jioni ya leo,February 29,2016,kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 
Panone FC walitangulia kwa bao bao la kichwa la beki wake wa kati, Godfrey Mbuda aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki kulia, Ayoub Masoud dakika ya 48 huku magoli ya Azam FC yakifungwa na Serge Wawa Pascal dakika ya 64 na dakika ya 77 kupitia kwa Mkenya, Allan Watende Wanga .

Azam FC inaungana na Yanga SC, Simba SC, zote za Dar es Salaam, Ndanda FC ya Mtwara, Coastal Union ya Tanga, Geita Gold ya Geita, Mwadui FC ya Shinyanga na Tanzania Prisons ya Mbeya kutinga Nane Bora ya Kombe la Azam Sports Federation 2016.

MATOKEO HATUA YA 16 BORA KOMBE LA TFF.


Leo; Februari 29, 2016.


Panone FC 1 - 2 Azam FC (Ushirika, Moshi)


Februari 28, 2016.


Simba SC 5 - 1 Singida United (Taifa, Dar es Salaam)


Toto African 0 - 1 Geita Gold (Kirumba, Mwanza)


Februari 24, 2016.


Yanga SC 2 - 1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)


Februari 26, 2016.


Ndanda FC 3 - 0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 


Coastal Union 1 - 0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)


Februari 27, 2016.


Mwadui FC 3 - 1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) 


Prisons 2 - 1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad