![]() |
|
Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi hapa nchini.
Mabadiliko
hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna
Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga
na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei
aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi
wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha
Kuzuia dawa za kulevya.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani
Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa
Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa
Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana
Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi
amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa
Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna
Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi yake
kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao
Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto
anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi
ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya
Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni
pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao
Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa
Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine
Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Mabadiliko
hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria,
kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera
Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)
Makao Makuu ya Polisi.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
Saturday, February 27, 2016
MABADILIKO JESHI LA POLISI TANZANIA:-Ni ya Makamanda wa Polisi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment