EPL 2015/2016:-Matokeo na Msimamo wa Ligi Kuu baada ya mechi za February 02,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, February 03, 2016

EPL 2015/2016:-Matokeo na Msimamo wa Ligi Kuu baada ya mechi za February 02,2016.

Wakiwa kwao Emirates Arsenal wametoka Sare 0-0 na Southampton na kubaki Nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza 2015/2016 huku Bao pekee la Sergio Aguero dakika ya 16, limeipeleka Manchester City nyuma ya Leicester City  kufuatia kuilaza Sunderland 1-0 Uwanja wa Light,usiku wa jana February 02,2016.

Pia Timu ya Leicester City imetanua mbawa zake kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Liverpool Uwanja wa King Power usiku wa jana.

Shukrani kwake mshambuliaji wa kimataifa wa England, Jamie Vardy aliyefunga mabao hayo dakika ya 60 na 71 na Leicester City sasa inafikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 24, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi zake 47.

Matokeo mengine ya mechi hizo na msimamo wa Ligi kuu ni kama ifatavyo hapa chini...''

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630-/+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad