Mkuu wa
Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo, Obedi Laiser
akijibu maswali ya waandishi wa habari
(Hawapo pichani) kuhusu gawio la mwaka huu
kwa watumiaji wa Tigo Pesa, kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John
Wanyancha.
Dar es
Salaam, Januari 13, 2016- Kampuni inayongoza katika kuleta maisha ya kidijitali
kwa jamii, Tigo, imetangaza tena malipo ya robo mwaka ya shilingi bilioni 4.4
(dola milioni 2.1) kwa watumiaji wake wa huduma ya Tigo Pesa wapatao milioni
4.6.
“Gawio hili
la faida linalipwa kwa watumiaji wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja binafsi,
mawakala wa rejareja na washirika wetu wa kibiashara, kila mmoja kutokana na
thamani ya fedha aliyojiwekea katika
akaunti yake ya Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya
Fedha kwa njia ya mtandao, Obedi Laiser.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Laiser amesema
kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza Tigo kuwalipa gawio la faida
watumiaji wa Tigo Pesa kwa mwaka wa 2016
akibainisha kuwa malipo hayo ni faida inayopatikana kutokana na amana ya
mfuko wa Tigo Pesa uliyowekezwa katika benki za kibiashara hapa nchini.
“Tunayo
furaha kubwa kutangaza gawio hili la faida kwa mara ya saba mfululizo tangu
tulivyoanza kufanya hivi mwaka 2014. Bila shaka hii inaonyesha ni jinsi gani
Tigo inajizatiti kuwaletea watanzania maisha bora ya malipo kwa njia ya
mtandao,” amesema Laiser.
Tigo ilikuwa
kampuni ya kwanza duniani kutoa gawio kwa wateja wake mwaka 2014
“Tunaamini
gawio hili la kwanza la faida ya Tigo Pesa kwa mwaka 2016 litakuwa ni kivutio
kikubwa kwa mamilioni ya watumiaji wa Tigo Pesa katika kufanikisha
mahitaji yao mbalimbali ya kifedha ya
mwanzo wa mwaka,” amesema Laiser.
Malipo haya
kwa watumiaji wa Tigo Pesa hutolewa kwa mujibu wa mwongozo wa Benki Kuu
uliotolewa mnamo Februari mwaka 2014. Mpaka sasa Tigo imelipa jumla ya 35.5bn/-
kwa wateja wake tangu kuanzishwa kwa utaratibu huu mwaka juzi na kampuni hiyo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment