TANROAD KAGERA:-Haya Mashimo Barabara ya Nyakanazi – Lusahunga –Rusumo yatatumaliza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 12, 2016

TANROAD KAGERA:-Haya Mashimo Barabara ya Nyakanazi – Lusahunga –Rusumo yatatumaliza.

.....Malori haya si yameharibika .....la hashaa...bali mashimo yanayosababishwa na uchakavu /ubovu wa barabara ya Nyakanazi- Lusahunga - Rusumo/Ngara  na hapa ni katika eneo la mteremko mkali wa Nyabugombe mpakani mwa Wilaya ya Ngara na Biharamulo mkoani Kagera,yalishindwa kupanda mlima huo na kuanza kurudi nyuma kutokana na kukwepa mashimo,utelezi ulioletwa na matope baada ya mvua kunyesha kama picha zinavyotuonesha.....hivyo kuleta ugumu wa kupitika.


Madereva wamekua wakipata wakati mgumu mara kwa mara pindi wawapo barabarani kwa kukwepa mashimo hayo makubwa yaliyopo katika barabara hiyo kuu ya kutoka Nyakanazi-Lusahunga kuja Benaco hadi Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Barabara hii inamashimo makubwa yaliyodumu kwa muda kadhaa,TANROAD muipitie barabara hii kwani inahitaji matengenezo kwa kuyaziba mashimo hayo ili kupunguza ajali zitokanazo na ukwepaji wa mashimo baadhi yaliyomo.



Hii ndio hali halisi iliyopo sasa kwa haya mashimo yaliyopo  barabara yanavyoonekana ,hali inayoleta ugumu wa magari yanayopanda mlima huo kupata wakati mwingine ajali au kukwama na kuteremka kwa sababu ya ubovu wa eneo hilo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad