Katika
mahojiano maalumu na Kituo Star TV, Kamanda Msangi amesema mwaka 2014 jumla ya
makosa 61,466 yamepatikana wakati mwaka jana makosa yalikuwa 76,346 ikiwa ni
ongezeko la makosa 14,898 ambapo kati yake mwaka 2015 makosa 71, 429 na 54,849
ya mwaka 2014 kwa pamoja yametozwa adhabu zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni
3 na Milioni 203 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Milioni 497.4 kwa tozo za mwaka
2014.
Kuhusu
Pikipiki za miguu miwili na mitatu maarufu kama na Bajaji, Kamanda Msangi
amesema ajali zake nazo zimeongezeka kutoka 141 mwaka 2014 mpaka 159 mwaka jana
ambazo kwa pamoja zimesababisha vifo 162 na kujeruhi watu 231 na kwamba nyingi
zimesababishwa na uzembe wa kukosa umakini kwa madereva.
Jiji la
Mbeya lina pikipiki za miguu mitatu zaidi ya 2100 wakati pikipiki za miguu
miwili ni zaidi ya 3000.
|
Tuesday, January 12, 2016
Home
HABARI
MATUKIO
TAARIFA / AJALI:-Watu 331 wafariki dunia mkoani Mbeya kwa ajali za barabarani 2015.
TAARIFA / AJALI:-Watu 331 wafariki dunia mkoani Mbeya kwa ajali za barabarani 2015.
Tags
# HABARI
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment