Wazanzibar
leo,January 12,2016 wanasherehekea miaka 52 ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964, ambayo
yaling’oa utawala wa Sultani kutoka Oman na kuwezesha wazalendo wengi kushika
hatamu ya kuongoza nchi.
Katika
kilele cha sherehe hizo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk Ali Mohamed Shein atahutubia taifa katika uwanja wa Amaan.
Atapokea
maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Unguja. Matukio mengine makubwa
yatakayofanyika katika uwanja huo ni Rais Shein kukagua gwaride la heshima la
vikosi ya ulinzi na usalama, vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) .
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na idara ya sherehe na mapambo iliyo chini ya Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais, sherehe hizo zitahudhuriwa na viongozi wa ngazi za
kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli ambaye ni mara ya
kwanza kushiriki baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka
jana,2015.
Ratiba hiyo
inaonesha kwamba sherehe hizo, zitahudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano na wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi aliwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi, yaliyowakomboa
wakulima na wafanyakazi kutoka katika kucha za wakoloni wa kisultani.
Aliwapongeza
wananchi kwa kujitokeza na kushiriki katika ufunguzi wa miradi ya maendeleo,
ambayo malengo yake ni kuharakisha maendeleo na kupambana na umasikini.
Mitaa
mbalimbali mjini hapa, imepambwa picha za viongozi mashuhuri waliosimama kidete
kufanya Mapinduzi hayo; hususan Rais wa Kwanza, Abeid Amaan Karume aliyeongoza
timu ya watu 16 kufanya mapinduzi hayo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment