|
Baadhi ya
kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa
Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza
mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.
|
|
Meneja
Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, akiongea na waandishi wa habari na
kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji
wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine
kulia kwake ni John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET)
na kushoto kwake ni Dkt. Flora Myamba
Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA.
|
|
|
|
Mkurugenzi
Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA, Dkt. Flora Myamba akiongea na waandishi wa
habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na
utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”.
Wengine toka kushoto John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa
mazingira(JET) na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas.
|
|
|
|
Meneja
Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Habiba Mtigino
kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni
ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia
mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”
|
|
|
|
Mkurugenzi
wa chama cha waandishi wa mazingira(JET), John Kikomo akionyesha kimoja kati ya
vyeti watakavyopewa kinamama walioshinda
shindano la kutunza mazingira wilayani Rufiji. Mpango huo ulidhaminiwa na Tigo
na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care
International.
|
|
|
|
Meneja
Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Mozza Salum kutoka
kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya
Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia
mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”
|
|
|
|
Baadhi ya
kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa
Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza
mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.
|
|
Itashirikana na REPOA, CARE INTERNATIONAL & KIDOGO KIDOGO.
|
Rufiji,
Desemba 23, 2015: Tigo imetoa simu za mkononi 200 ambazo zitasambazwa kwa
wanawake maskini ambao hawana uwezo wa kununua simu katika wilaya ya Rufiji
mkoani Pwani, lengo kuu likiwa ni kuziba pengo la kijinsia katika umiliki wa
simu Tanzania.
Usambazaji
wa simu hizo upo chini ya programu inayojulikana, “Mradi wa Kuwaunganisha
Wanawake” utafanyika kwa kushirikiana na asasi tatu zisizo za serikali za
REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.
Akizungumzia
zoezi hilo Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, alisema kwamba
mtazamo wa Tigo uko kwenye sera za kampuni ya kuwawezesha watu walio na kipato
duni ndani ya jamii katika kuzipata simu za mkononi.
“Tigo inadhamiria kuboresha muunganisho wa simu za
mkononi nchini Tanzania hususani
miongoni mwa wanawake ambao kimsingi
wana uwezo mdogo wa kupata simu,” alisema Bi.Thomas na kuongeza, “Ni matumaini
yetu kwamba kwa kusambaza simu hizi kwa
wanawake maskini katika wilaya ya Rufiji, Tigo itakuwa imechangia
kupunguza pengo la kijinsia katika
umiliki wa simu nchini.”
Thomas alisema kwamba Tigo imewekeza zaidi ya
dola 30,000 ambazo zitatumika kusambaza
pamoja na kuangalia tathmini ya matokeo ya mradi. Aliongeza kwamba
washirika watatu REPOA, CARE International na KIDOGO KIDOGO kwa pamoja
wataongoza utekelezaji huo wa usambazaji wa simu kwa kutoa laini ya simu pamoja
na kufanya tathmini ya matokeo ya mradi.
“Pengo
lililopo la kijinsia katika kuifikia teknolojia ya simu linaweza kukwaza
Tanzania katika mchakato wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika
kukuza usawa kijinsia na kuwawezesha wanwake nchini na ndio maana Tigo
inachukua hatua za kuunga mkono mradi huu,” alisema Bi.Thomas.
Kwa mujibu wa Bi. Thomas mradi huo unalenga
kuwanufaisha watu 500 katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016 na inakuwa ni mara
ya pili kwa Tigo kusambaza simu za
mkononi kwenye mkoa huo kwani mara ya kwanza ilikuwa amwaka 2014.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
No comments:
Post a Comment