Amis Tambwe
akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo wa leo kati ya Yanga
dhidi ya Stand United.
Tambwe
alianza kuzifungua nyavu za Stand United dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri
iliyofanywa na kiungo mshambuliaji Thabani Kamusoko.
Mrundi huyo
hakuishia hapo kwani dakika ya 36 alizama tena nyavuni kupachika bao la pili
kwa kichwa na kuifanya Yanga iendelee kuongoza kwa goli 2-0 mbele ya ‘wapiga
debe’ wa mjini Shinyanga.
Wakati
mchezo unaelekea mapumziko Yanga walifanya shambulizi la kushtukiza ambapo
mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alimiliki mpira kisha kumuwekea mpira Tambwe
ambaye moja kwa moja aliachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Stand
United Frank Muwange na kujaa wavuni dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Thabani
Kamusoko aliyefunga bao pekee la Yanga wakati ikiwa mkoani Tanga, alifunga bao
la nne kwenye mchezo wa leo dakika ya 62 kipindi cha pili na kuipa timu yake
ushindi mnono kwenye mchezo wa leo.
|
Tambwe
(katikati) akipongwewa na wachezaji wenzake wa Yanga Deus Kaseke (kushoto) na
Simon Msuva (kulia)
Ushindi huo
unawapa Yanga SC nafasi ya kuendelea kukaa kileleni mwa VPL wakifikisha jumla ya
pointi 30 baada ya kushuka dimbani mara 12 msimu huu wakati Stand United wao
wamepoteza mchezo wa pili mfululizo baada ya kupigwa kwenye mchezo uliopita wa
‘Shinyanga Derby’ dhidi ya nduguzao Mwadui FC.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
No comments:
Post a Comment