Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera
John Bulimba – SSP.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI. Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi. Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jeshi la polisi, vyeti feki vyawaondoa askari kazini’ Taarifa hiyo ni uzushi na haijatolewa na Jeshi la Polisi. Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii. Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumia mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii. Imetolewa na: Advera John Bulimba – SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi. Makao Makuu ya Polisi. Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
Saturday, December 19, 2015
JESHI LA POLISI:- Vyeti feki vyawaondoa askari kazini ni Uzushi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment