Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na mmoja wa watendaji wa
wilaya ya Ikungi mkoani Singida mara tu alipowasili kijiji cha Puma
kukagua mradi wa ufugaji kuku wa kusaidia watu wanaoishi na VVU
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia
TACAIDS. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.
Na Modewjiblog team, Singida
MRATIBU
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Bw.Alvaro Rodriguez ameipongeza
serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira yanayofanikisha miradi
mbalimbali ya maendeleo endelevu.
Mratibu
huyo alitoa wito huo wakati alipofanya ziara ya siku mbili mkoani
Singida kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Baada
ya kuona mafanikio katika miradi hiyo Bw. Rodriguez, alisifu pia jamii
ya Singida kwa kujitoa kuhakikisha kwamba wanafanikisha miradi hiyo kwa
kuifanya kuwa miradi yao.
Katika
ziara hiyo ambapo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone na Afisa
wa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa Wizara ya
Mambo ya Nchi za Nje, Bi. Maulidah Hassan walikuwepo, Mratibu
alitembelea kituo cha watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi; Kituo cha
kutibu kipindupindu na Ushirika wa wajasiriamali vijana.
Miradi
hiyo inafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDS).
UNAIDS ni mshirika wa karibu wa serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia mashirika ya TACAIDS na ZAC.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Puma
kukagua mradi wa kikundi cha ufugaji kuku kwa watu wanaoishi na VVU.
Mashirika ya TACAIDS na ZAC yanatambulika kitaifa na kimataifa kutokana na shughuli zake za kuhudumia umma wa Tanzania.
Miradi hiyo imewezesha vijana wengi kuwa wajasiriamali, kudhibiti Kipindupindu na kuongeza uelewa wa UKIMWI.
Alisema
kwamba maendeleo endelevu yanahusisha serikali na jamii kuangalia
changamoto zinazokabili jamii na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuoanisha na
malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Miradi hiyo iliyopo Singida inatekelezwa chini ya mpango wa msaada wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).
Mashirika
ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanywa shughuli mbalimbali za kusaidia
wananchi wa Tanzania waume, wake na watoto kupitia mpango wa msaada wa
maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP) wa mwaka 2011-2016.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Kone akisisitiza umuhimu wa wananchi
kujimilikisha miradi hiyo, amewaambia Umoja wa Mataifa kwamba kwamba
wananchi wa mkoa huo wataendelea kujimilikisha miradi hiyo na kuifanya
ya kwao ili kuharakisha maendeleo endelevu.
Mkuu
wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Chigulu Charles (wa kwanza kulia)
akitoa taarifa yake ya mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi
vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI wilayani humo. Wa tatu kushoto,ni
Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na wa pili kushoto ni Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone.
Alisema
maelfu ya wananchi wa Singida wamenufaika na miradi ya maendeleo
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake yaliyopo hapa
nchini .
Aidha
alitaka Mashirika hayo kuendelea kusaidia miradi mbalimbali na hasa
wakati Mpango wa pili wa Msaada wa maendeleo (UNDAP II) unapokaribia
kuanza mwakani, sanjari na mpango wa maendeleo wa taifa Julai 2016.
Alisema
Singida imesonga mbele katika maendeleo katika siku za karibuni lakini
bado inahitaji msaada wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kuendelea
kuhifadhi mafanikio na kuyaboresha.
Mhudumu
wa watu wanaoishi na VVU kata ya Puma tarafa ya Ihanja wilaya ya
Ikungi, Kelvin Mwiru, akitoa taarifa yake juu ya majukumu ya kuhudumia
watu 150 wanaoishi na VVU katika vijiji vya kata ya Puma na vijijini
jirani.Mhudumu huyo ameiomba halmashauri ya wilaya ya Ikungi na wadau
wengine kumtambua na kumpa ushirikiano katika kazi hiyo ngumu ya
kujitolea kuwahudumia watu wanaoishi na VVU ambao wanaongezeka kila
kukicha.
Mratibu
mkzi wa mashirka ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (anayengalia kamera) akitoa
nasaha zake mbele ya kikundi cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu
wanaoishi na VVU na wananchi kwa ujumla wa kijiji cha Puma wilaya ya
Ikungi.Mwenye suti ya bluu, ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko
Kone.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.
Parseko Kone wakiangalia baadhi ya kuku wa mayai walipotembelea kikundi
cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU na wananchi kwa
ujumla wa kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dkt. Parseko Kone (kulia) pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Maulidah Hassan (katikati) wakitazama mayai
yanayototolewa na kuku hao.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.
Parseko Kone, Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Chigulu Charles (kulia), Afisa
wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan na Mratibu
wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala Fedes katika picha ya pamoja na baadhi
ya wanakikundi cha ufugaji kuku cha Upendo cha watu wanaoishi na VVU.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akiondoka katika kijiji cha Puma kuelekea kijiji cha Mandewa kilichopo Singida mjini.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mganga mfawidhi wa
manispaa ya Singida, Dk. John Mwombeki baada ya kuwasili kwenye kambi ya
muda ya wagonjwa wa Kipindupindu iliyopo katika kijiji cha Mandewa nje
kidogo ya mji wa Singida akiwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dkt. Parseko Kone.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiingia kwenye kambi ya muda ya
wagonjwa wa kipindupindu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni katika
kambi ya wagonjwa wa Kipindupindu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwaeleza jambo mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) na Afisa kutoka Shirika la
Afya (WHO) kanda ya Dodoma, Dk. Cyrialis Mutabuzi (kulia) pamoja na
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania
Hoyce Temu (wa pili kushoto).
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone akizungumza na mgonjwa wa
kipindupindu kutoka kijiji cha Mtavila wilaya ya Ikungi, Jumanne
Shaban. Dkt. Kone amemuagiza akirudi kijijini akawe Balozi mzuri wa
mapambano dhidi ya kipindupindu.WHO inasaidia uendeshaji wa vituo hivi pamoja na tiba.Kwa matukio ya picha zaidi Bofya hapa
No comments:
Post a Comment