Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto
ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama
alivyonaswa na kamera yetu.
|
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake
aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia
Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya
Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita
kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul
Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA
ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi
kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani
Kigoma.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati
akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara
yake mkoani Kigoma.
Alisema
kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma
wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya
Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya
wakimbizi.
Alisema
Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania
inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za
kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao
wakati hali ilipokuwa njema.
Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.
Alisema
Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano
katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia
kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao
waweze kuishi kwa amani.
Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea
ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
Alisema
kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi
ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za
shule, afya, maji na mengine.
Aidha
wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya
Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa
upendo kwa majirani zake.
“Dunia
ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa
hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane”
alisema mratibu huyo.
Akizungumza
kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa
yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa
huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika
hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi
hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi
makwao.
Tanzania
imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya
Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara,
maji, vituo vya afya na shule.
Katika
ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya
Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani
ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.
ILO
Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la
kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha
kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
Katika
msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia
Wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo
kamera).
Alisema
kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua
fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya
familia zao.
“Naona
uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao
kuondokana na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi
na kuondoa changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema
mratibu huyo.
Mkoa
wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi
mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika
hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma
ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya
Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la
Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la
Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)
na Shirika la maendeleo (UNDP).
Akizungumza
Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia
Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya
Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha
kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru
Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.
“
Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima
nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na
matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
Ofisa
wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga
picha kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa
Wakimbizi nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu hali ya
kambi ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na wakati msimu
wa masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa ikaharakisha
kukamilisha miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.
Serikali
imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na Ntendeli, Kakonko
kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi hiyo.
DC
huyo pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na lazima
wadau wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa pamoja
na kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.
Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.
Aidha
alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana baadhi yao
wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na polisi
kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
Kuwepo
kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa mazingira kama
inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni kwenye misitu
iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Aidha
katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma inavyotoa
ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya maendeleo
na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa Shirika la
mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alisema
kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano huo.
Alisema
anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la Tanzania kuwa bora
zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya serikali,
mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa linapokea
elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.
“Taifa
la Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini yake, taifa
hili lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na ushirikiano
wenye lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi” alisema
Kanem.
Anasema
kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja na mashirika
ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo ya
ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya
kufanikisha maendeleo.
Alisema
UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa vijana
mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha ustawi wa
jamii na taifa kwa jumla.
Aidha
alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa elimu hivyo
kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa uelewa miongoni
mwa jamii.
Mratibu
huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake wamerejea Dar
es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja wa Mataifa
inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.
Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.
Katika
ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo inavyobadili jamii
husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya
maendeleo nchini Tanzania.
Mkuu
wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea changamoto
mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa
Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto)
kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa Mambo ya Nje
kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi mambo muhimu
wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile
(hayupo pichani).
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye mkutano wa
kupokea taarifa ya kambi hiyo.
Kutoka
kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes Mwangoka,
Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce
Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na Ofisa wa Mambo ya
Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakielekea kwenye kambi
za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini,
Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya
wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini,
Dkt. Natalia Kanem wakiuliza jambo kwa Ofisa Mtafiti Mshirikishi wa
ofisi za UNHCR, Kasulu, Mariam Khokhar walipotembelea ndani ya mahema
wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya
Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wa pili kushoto ni Mkuu
wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Eneo la mahema ya kulalia familia za Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu.
Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.
Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
Mtoto
ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto
ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama
alivyonaswa na kamera yetu.
Moja
ya familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia msafara
wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea kambini
hapo mwishoni mwa juma.
Ofisa
wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipozi na
moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa kambi ya
Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara yake ya
kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.Kwa matukio zaidi ya picha bofya link hii
No comments:
Post a Comment