Ofisa
Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas
(kushoto) akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Tabora.
Pichani wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah
Hassan (wa tatu kushoto) wakipitia taarifa hiyo kwa pamoja kabla ya
kuelekea kukagua miradi hiyo.
Na Modewji blog team, Tabora
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Mipango ya Maendeleo la Umoja huo Bw.Alvaro Rodriguez, amesema kwamba
umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo katika mkoa wa
Tabora yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
Hayo alisema jana baada ya kuzuru miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Tabora.
Miradi
hiyo ni ya ujenzi wa bwawa la nguvumoja kwamtindo wa utoaji wa chakula
kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya miyombo.
Katika
ziara hiyo ambayo alikuwa na Ofisa kutoka Kitengo cha ushirikiano wa
kimataifa wizara ya mambo ya nchi za nje, Bi. Maulidah Hassan Mratibu
huyo aliridhishwa na mafanikio ya miradi hiyo ambayo imelenga kupiga
vita umaskini na kutunza mazingira.
Ziara
ya Mratibu huyo mkoani Tabora ni moja ya ziara yake ndefu ya
kutembelea miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika
mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.
Alipotoka
Singida jana asubuhi alifika katika moja ya Wilaya kame nchini, Wilaya
ya Igunga na kuona mradi unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula
la Umoja wa Mataifa (WFP) wa ukarabati wa bwawa la Charco.
Bwawa
hilo ambalo litahudumia watu takribani 6,100 kutoka vijiji vya
Nguvumoja, Ndembezi na Iborogelo lilijengwa awali na miradi ya TASAF
lakini wakati wa mvua za Elnino tuta lake lilivurugika vibaya.
Akizungumzia
bwawa hilokaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga ambaye pia ni Ofisa
Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas, akizungumza
alisema kwenye bwawa hilo kwamba Umoja wa Mataifa kupitia WFP
wanawezesha ukarabati wa bwawa hilo kwa kutoa chakula kwa wachimbaji.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) aliyeambatana na
Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa
pili kushoto) walipowasili kukagua mradi wa ujenzi wa
Bwawa la Charco la Nguvumoja kwa mtindo wa utoaji wa chakula kutoka
Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa kazi inayofanywa na mradi wa
misitu ya Miyombo. Kushoto ni Ofisa Tawala msaidizi anayeshughulikia
Uchumi na Tija wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Dkt. Phillips Mtiba
pamoja na Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga,
Samaluku Joseas (wa pili kulia).
Aidha
imeelezwa kuwa tuta hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia
kaya 1,200 na Ng’ombe elfu moja na kuweza kuhifadhi maji kwa mwaka
mzima.
Imeelezwa
kuwa wajenzi wanapewa debe moja la Mahindi kwa kina cha mita moja na
urefu wa mita nne na upana wa mita tatu na nusu lita ya mafuta ya kula
na Njegere kilo tatu.
Kumalizika kwa bwawa hilo kutasaidia kupunguza umbali wa wananchi katika kutafuta maji.
Awali wananchi walilazimika kusafiri kilomita 30 kupata maji katika bwawa la Manzugi kuchota maji na kunywesha mifugo.
Aidha imeelezwa kuwa baadae wanyama watatengewa eneo la kunywa maji.
Aidha
alitembelea kikundi cha ufugaji nyuki, utunzaji wa mazingira pamoja na
usindikaji wa matunda pori cha Membo , wilayani Uyui.
Kikundi
hicho kilichopo wilayani Uyui kimeanzishwa Mei 8,2007 na Katibu wa
kikundi Nasibu Baraka alisema kikundi hicho chenye wanachama 30
kimefanyakazi kubwa ya kupiga vita umaskini.
Alisema
ili kukabiliana na adui njaa na umaskini kikundi hicho kwa ufadhili wa
UNDP kimewezesha kujiajiri wenyewe, Kusindika matunda ya asili kwa ajili
ya jamu na divai,kilimo cha bustani, kilimo cha chakula na biashara,
ujenzi wa majikobanifu,usagaji wa unga na kupika keki za Muhogo mbichi
kwa Karanga na Asali.
Akisoma
risala kwa Mratibu wa UN Tanzania alisema kwamba wamekuwa na mafanikio
makubwa kutokana na ruzuku mbalimbali za UNDP ikiwamo mafunzo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea kupata maelezo ya mradi
huo.
Aidha amesema kwamba kwa sasa wanatumia sola badala ya mafuta ya taa huku mradi wa Miyombo ukiendelea kuleta neema.
Aidha ametaka umoja huo kuwasaidia kuwa na mshine za kisasa cha kusindika matunda na chakula.
Viongozi
hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo
unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa
Umoja wa Mataifa,(UNDAP).
Aidha
mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya
uragibishi na na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na
utunzaji wa mazingira.
Naye
Ofisa utawala msaidizi wa mkoa anayeshughulikia Uchumi na Tija Dk.
Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Tabora, Ludovick
Mwananzila ambaye hakuwepo kutokana na majukumu mengine kwenye mikutano
na wananchi kuhusu miradi ya TASAF, alisema baada ya kumaliza kukagua
miradi kwamba wameridhika na miradi inayofadhiliwa na UN katika mkoa
huo.
Alisema
pamoja na kwamba walitembelea miradi michache lakini ni dhahiri mkoa wa
Tabora umefurahishwa na misaada iliyotolewa ambayo inatia moyo na
kusaidia harakati za serikali za kukomboa wananchi wake kutoka katika
lindi la umaskini na ukosefu wa huduma muhimu kama za maji na hifadhi ya
mazingira.
Pamoja
na kushukuru kwa misaada hiyo kwa wanatabora na maendeleo yao, alitaka
UN isiwachoke kusaidia vipaumbele vya mkoa huo ambavyo ni kujitokeza kwa
chakula na hifadhi ya misitu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na ukaguzi wa Bwawa hilo.
“
Nashukuru sana kwa msaada tunaoendelea kupata kutoka UN kwa ajili ya
maendeleo ya wana Tabora na Tabora kwa ujumla na niseme tu kwamba kama
wana Tabora kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na mengine hatuwezi
kuyafanya na hapo ndipo sasa tunapoweza kuona umuhimu wa nafasi ya
wafadhili na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo.” Alisema Dk.
Phillips.
Alisema
ingawa walikuwa na muda mfupi na kutembelea miradi michache , alitamani
waje kurudi kuona miradi mingi zaidi ili watambue kwamba miradi hiyo
inabadilisha wana Tabora na hawachezei fedha za ufadhili.
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
Alisema
suala la uhakika wa chakula kwa wananchi ni muhimu kwao kutokana na
ukweli kuwa wananchi wakiwa na chakula hata fedha zao zitakaa mfukoni na
kufanya kazi nyingine za maendeleo. Alisema kutokana na hali hiyo
wataendelea kuomba kusaidiwa katika eneo hilo.
Aidha
alitaka mkoa wa Tabora kuendelea kusaidiwa kutunza misitu ya Miyombo
kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa misitu ni
kivuta mvua na maji ndio pembejeo namba moja katika uzalishaji wa
chakula.
Alishukuru
UNDP kwa kusaidia kuhifadhi misitu hiyo ili kuwapo na uvunaji endelevu
kwa kusaidia jamii kuitunza na kuismamia rasilimali hiyo na kuitumia
katika fursa za kiuchumi kama ufugaji nyuki.
Leo Mratibu huyo ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Kigoma.
Wananchi wakiendelea kuchimba bwawa hilo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Nguvumoja watakaonufaika na mradi wa bwawa hilo.
#HapaKaziTu; ndio maneno aliyokuwa akiyasema Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akichimbia sehemu ya bwawa
hilo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wa Bwawa la Charco la
Nguvumoja.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akichimba udongo na sururu huku Afisa
wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akijaza
udongo unaochimbwa kwenye ndoo.
Mratibu
Mkazi wa UN nchini Bw. Rodriguez akimwaga udongo aliokuwa akichimba
katika bwawa hilo ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
wanachi wa kijiji cha Nguvumoja katika Halmashauri ya Igunga.
#HapaKaziTu; Wanakijiji
pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakishangilia kwa
pamoja huku wakiunga kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli ya #HapaKaziTu sambamba
na mabango 17 ya malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development
Goals-SDGs) walioyowafikia wanakijiji wa Nguvumoja. Kwa matukio zaidi bofya link hii
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
No comments:
Post a Comment