Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akiongozana na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara tu baada ya kumpokea alipowasili
ofisini kwake akiwa ameongozana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (hawapo
pichani).
Na Mwandishi wetu, Kigoma
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameelezea kufurahishwa kwake
na uwapo wa mradi wa kusaidia vijana wa kitanzania kujifunza ujasirimali
na kujitegemea.
Akizungumza
katika shughuli za uzalishaji mali za vijana wa Shirika lisilo la
kiserikali la Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma
alisema kwamba shughuli wanazofanya vijana hao zinamsisimua sana.
“Tunafurahi
sana mimi na wenzangu kutembelea mradi huu unaofadhiliwa na Shirika la
Kazi Duniani (ILO) ambao unachochea ujasirimali miongoni mwa vijana.
Sote tunajua kwamba vijana wengi wa Kitanzania wanaume kwa wanawake
wameelimika lakini hawana ajira rasmi.
Na suala la ujasiriamali ni kitu
ambachio mtu anaweza kujifunza, na ujasiriamali unatoa fursa kwa vijana
kujiunga katika kundi la wafanyakazi kwa kujiajiri wenyewe.
“Tunajua
kwamba kupitia shughuli zinazofadhiliwa na ILO katika ngazi ya jamii na
kwa kufuata maelekezo ya serikalai za mtaa vijana wanaanzisha biashara
mbalimbali binafsi au na jamii. Kiwanda cha kutengeneza sabuni ni mfano
mzuri sana.
Tunaona kwamba mradi huu unawaongezea kipato na hivyo kuweza
kusaidia familia zao na kupeleka watoto shuleni na kuboresha lishe .
Kwa ufupi mradi kama huu unasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazokabili kaya maskini Kigoma” alisema Rodriguez
ILO
Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la
kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha
kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya (kushoto)
akibadilishana 'Business card' na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa
idadi ya watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem.
Alisema
kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua
fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya
familia zao.
Aidha
alisisitiza haja ya jumuiya ya kimataifa kuusaidia mkoa Kigoma katika
nyanja mbalimbali za kiuchumi hasa katika eneo la ajira kwa vijana
kutokana na ukarimu wa wakazi wa mkoa huo katika kuwapokea na
kuwahudumia wakimbizi kutoka nchi za maziwa makuu kwa upendo.
Rodriguez
alisema pamoja na ombi hilo Mratibu huyo wa shughuli za kimataifa
ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
alisema wao kama UN wakifanyakazi pamoja wataendelea kutoa misaada kwa
wakimbizi hasa uanzishaji wa miradi ya kiuchumi kwa vijana na wanawake.
Kwa
upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Idadi ya
watu (UNPFA), Dkt. Natalia Kanem alisema kuwa kupatiwa mitaji na
kuanzisha vikundi vya uzalishaji kwa vijana na wanawake kunasaidia
kuongeza ajira lakini pia kusaidia kupunguza ongezeko kubwa la idadi ya
watu bila mpangilio.
Katika
risala yao kwa uongozi huo wa Umoja wa Mataifa vijana kutoka Nyakitonto
Youth Development Tanzania wamesema kuwa misaada iliyotolewa kwao
imewasaidia kupata ujuzi na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ikiwa ni
sehemu ya kujiajiri na kujiongezea kipato ili waweze kuendesha maisha
yao bila utegemezi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akitoa taarifa ya mkoa
wake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe
ofisini kwa Mkuu huyo wa mkoa.
Hata
hivyo vijana hao katika risala yao iliyosomwa na Meneja miradi wa
shirika hilo, Anjelina Gulanywa walisema kuwa pamoja na mafanikio hayo
wanakabiliwa na changamoto utaalam mdogo, mitaji na vitendea kazi vya
kisasa ili kufanya shughuli zao kuwa na mafanikio zaidi.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya alieleza
kuridhishwa kwake na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kusaidia miradi
mbalimbali mikoani mwake ambayo inasadia wananchi kukabiliana na
umaskini.
Mkoa
wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi
mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika
hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma
ni pamoja na Shirika la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR),Shirika la Afya
Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Idadi ya watu (UNFPA) ,Shirika la
kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia watoto( UNICEF), Shirika
la Kuhudumia wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani
(WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake
katika mkoa wa Kigoma kwa Mkuu wa mkoa huo, Kanali Mstaafu, Issa
Machibya.
Afisa
Mawasiliano wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) nchini, Magnus Minja
akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa
vijana yenye lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumai
familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana
na kipato chao unaofadhiliwa na shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwasilisha Malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu (Sustainable Development Golas-SDGs) kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la
Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi ya Khanga ya 'miaka
60 ya UNFPA Tanzania', kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanal Mstaafu, Issa
Machibya, huku Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA)
nchini, Dkt. Natalia Kanem akishuhudia tukio hilo.
Malengo
ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia Kigoma. Pichani ni Mkuu wa mkoa
wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya na baadhi ya wakurugenzi katika
ofisi ya mkuu huyo wa mkoa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Umoja
wa Mataifa Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
Mkuu
wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya akiagana na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake kabla ya
kuelekea kambi ya wakimbizi Nyarugusu.
KUELEKEA KWENYE UKAGUZI WA MRADI WA VIJANA UNAORATIBIWA NA ILO........
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la
Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakisikiliza
taarifa ya waratibu wa mradi wa Vijana unaoratibiwa Shirika la
Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma (NYDT) na
kufadhiliwa na ILO katika kuwawezeshaji vijana masuala ya ujasiriamali.
Meneja
miradi wa shirika hilo, Anjelina Gulanywa, Angelina Guranywa akitoa
taarifa kwa Mkuu wa UN Tanzania (hayupo pichani) na ugeni wake
alioambatana nao.
Malengo
ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia Shirika lisilo la kiserikali la
Nyakitonto Youth For Development Tanzania mkoani Kigoma.
Baadhi ya vijana walionufaika na mradi wa ILO wa kuwezesha vijana kuwa wajasiriamali kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali.
Mratibu
wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto for Youth Development
Tanzania, Joel Nyakitonto, akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),
Alvaro Rodriguez jinsi utengenezaji wa sabuni kutokana mafuta ya mbegu
za Mchikichi walipotembelea kiwanda cha Sabuni kilichopo tarafa ya
Katubuka ambacho kinamilikiwa na kijana Diocres Dionizi (hayupo pichani)
ambaye ni mmoja kati ya vijana 30 aliyenufaika na mafunzo ya Anzisha
Biashara Yako (ABIYA) yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa ufadhili wa
Shirika la Kazi nchini (ILO).
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakikusanya mbegu kwa ajili ya kukamuliwa kwenye mashine maalum.
Ofisa
wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akimtwisha
ndoo ya mbegu za Mchikichi zinazokamuliwa na kupatikana mafuta
yanayotengenezea sabuni za magadi mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho
ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi.
Mwakilishi
wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia
Kanem akimsaidia kujaza mbegu za Mchikichi mmoja wa wafanyakazi
kiwandani hapo kwa ajili kuzichuja na kupata mafuta yanayotengenezea
sabuni za magadi.
Mwanamke
aliyebeba mtoto wake mgongo huku akiwa amejitwishandoo yenye mbegu za
Mchikichi kuelekea ndani ya kiwanda cha kusaga mbegu hizo zinazotoa
mafuta yanayotumika kutengeneza sabuni za magadi kiwandani hapo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akivaa koti maalum kwa ajili ya
kuingia kiwanda kujionea jinsi kijana huyo anayotengeneza sabuni za
magadi zinazotokana mafuta ya mchikichi. Kushoto mmiliki wa kiwanda
hicho kijana Diocres Dionizi aliyenufaika na mafunzo ya ABIYA
yaliyofadhiliwa na ILO.
Mfanyakazi
wa kiwanda hicho kitengo cha ufungashaji bidhaa, Eric Mwesiga (27)
akimwelekeza Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Maulidah Hassan (kushoto) namna wanavyopakia sabuni hizo kwenye mifuko
maalum tayari kuingia sokoni.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa
idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakishuhudia
maandalizi ya utengenezaji wa sabuni kiwandani hapo.
Maandalizi yakianza kwa kumimina mafuta yaliyotokana na mbegu za mchikichi.
Kijana
Diocres Dionizi aliyenufaika na mafunzo ya ABIYA yaliyofadhiliwa na ILO
akisaidiana na mfanyakazi wake Erick Mwesiga kumwaga mchanganyiko huo
kwenye chombo maalum huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akishuhudia tukio hilo.
Erick Mwesiga akichanganya rangi kwenye mchanganyiko ambao unakaa siku tatu mpaka kukauka na kupatikana sabuni za magadi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa
idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem katika picha ya pamoja
na Baba mzazi wa kijana Diocres Dionizi ambaye ni mjasiriamali wa
sabuni.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwasili kuzindua eneo la heka 3 la
rasilimali na kuwaanda vijana (Youth incubation centre) ambalo
limetolewa na manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Taasisi isiyo ya kiserikali
ya Nyakitonto Youth For Development Tanzania wanaojihusisha na kutoa
mafunzo mbalimbali ya masuala ya ujasiriamali ikiwemo kuanzisha
biashara.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikata kuzindua eneo la heka 3 la
kituo cha mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya kuwaanda vijana katika kilimo
na ufugaji kuku (Youth incubation resource centre) ambalo limetolewa na
manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Nyakitonto
Youth For Development Tanzania kwa faida ya vijana Kigoma kujikwamua
kiuchumi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipata maelezo ya eneo la ndani
litakalotumika kwa vitendo katika kilimo na ufugaji kwa vijana wa Kigoma
ili waweze kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment