Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa amewataka wananchi waendelee kulinda amani ya nchi huku
akikemea uvaaji wa nguo fupi na kuwasihi Watanzania kujenga tabia ya kuvaa
mavazi yenye kumpendeza Mungu.
Pia,
amekemea matumizi ya dawa za kulevya na mimba za utotoni akisema ni mambo
ambayo yanaepukika kwa mtu yeyote aliyelelewa katika misingi ya kidini.
Waziri
Majaliwa alisema hayo jana December 24,2015, alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid lililofanyika
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Alisema
mambo yote hayo yanawezekana kama watu watamkimbilia Mungu huku akiwaomba
viongozi wa dini kuwausia waumini wao kuvaa mavazi ambayo yanampendeza Mungu.
“Mtoto
akilelewa kwenye mazingira ya dini itakuwa ngumu kuvaa mavazi ambayo
hayampendezi Mungu,” alisema.
Amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini zile ambazo ziko kisheria
huku akizitaka ziendelee kuisaidia Serikali kwa kujenga shule na hospitali na
kutoa huduma nyingine za kijamii.
Waziri
Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwapongeza Watanzania kwa kuwa watulivu katika
kipindi chote cha uchaguzi hadi ulipofanyika Oktoba 25,2015.
Akizungumza
katika baraza hilo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Abubakari Zuberi aliwaasa
waumini wa Kiislamu kufanya mambo yote yanayompendeza Mwenyezi Mungu.
Aliwashukuru
Waislamu wote nchini kwa kushirikiana na wananchi wenzao ambao siyo wa dini
hiyo katika kudumisha amani.
|
No comments:
Post a Comment