Anna
Alphonce (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busolo akifafanua
jambo wakati akielezea uraghbishi anaofanya.
Akiwa kama
mwenyekiti mwanamke wa kitongoji aliweza kutumia nafasi yake kufanya uraghbishi
kwa anaowaongoza. Kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu,
aliitisha mikutano kwenye kitongoji chake kwa lengo la kutoa hamasa ya wananchi
kujitokeza kwa wingi.
Kwa nafasi yake aliweza kuyafikia makundi ya wazee,
vijana na wanawake. Ingawa kati ya hawa wanawake ndio walikuwa washiriki
wazuri.
“Msisitizo
kwenye mikutano yangu ilikuwa ni kupiga kura kwa amani. Niliwasihi Vijana wetu
wasiwe chanzo cha vurugu na badala yake wawe walinzi na kuhakikisha uchaguzi
unafanyika katika mazingira ya utulivu,”Haya ni
maelezo ya mwenyekiti huyo akielezea jinsi alivyotumia nafasi yake kwenye
kufanya hamasa ya amani. Akaongeza,“Kwangu mimi
haya ni mafanikio kwa sababu kweli uchaguzi umefanyika kwa amani katika
kitongoji change.”
Mraghabishi
mwingine ni Matrida Peter toka katika kijiji cha Nyandekwa, yeye uraghbishi
wake alifundishwa na Elizabeth Ngaljalina toka kijiji hicho hicho. Baada ya
kufundishwa yeye alichoamua kufanya uraghbishi kwa vijana wa kijiji cha
Nyandekwa pamoja na wale waliokuwa mashuleni pia.
Akielezea
jinsi ambavyo anafanya uraghbishi kwa vijana, Matrida anasema,“Nafundisha
makuzi ya ujana ili kuweza kutimiza ndoto zao. Kwanza nawaelewesha kuhusu mabadiliko
ya miili yao hasa wanapoingia hatua ya kubalehe na kuvunja ungo. Hii
inawasaidia jinsi ya kujikinga na maambuzi ya virusi vya ukimwi.”
Uraghbishi
wake hauishii kwa vijana walio nje ya shule, hivyo alikwenda kumtembelea ili
aweze kupata fursa ya kutoa elimu hiyo hasa kwa wanafunzi ya shule ya msingi.
Walengwa wakubwa wakiwa ni wanafunzi wa kuanzia darasa la nne mpaka la saba.
Akielezea rika la watoto hao, Matrida anasema:-“Watoto wa
siku hizi wana maumbo makubwa, hivyo hao wa darasa la nne mpaka la saba sio
wadogo kiumbo na wengi ndio wapo kwenye huo umri.
Wanahitaji mwongozo manake
makuzi siku hizi yameachwa kwa wazazi na wao mda mwingine wanaona aibu kuongea
nao,”Matokeo ya
uraghbishi huu wa mwanamama Matrida ni kuongeza kwa watoto wenye uelewa wa
mipango ya uzazi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Kwani maambukizi katika
wilaya ya Kahama yapo juu kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.
Uraghbishi
una maana tofauti tofauti kwa wanawake hawa wa kijiji cha Nyandekwa, kama
anavyoelezea Mariam Stephano aliyeanza uraghbishi mwezi Septemba 2015:-“Uraghbishi
kwangu mimi ni kutetea haki za vijana na mabinti, na sio tu kutetea bali kujua
na falsafa yake ya jinsi ya kutenda ili kufanikisha lengo hilo ninaloliangalia
kama ndio jukumu langu,”
Wakati Suzan
Stephano yeye analinganisha uraghbishi na haki za kikatiba. Huku akisisitiza
umuhimu wa kuthaminiwa kwa mwanamke katika kijiji chao na taifa kwa ujumla. Na
yeye pia anakiri kwa uraghbishi ni falsafa ya jinsi ya kutenda.
|
No comments:
Post a Comment