Makosa ya Mtandao.
Ni mojawapo ya maeneo ya changamoto kwa Rais Dk. Magufuli, baada ya serikali ya Marekani kuiwekea vikwazo Tanzania, ikihitaji maelezo ya kina kuhusu watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni, wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Sheria hiyo iliyoanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu na tayari imeshawatia matatani wa kadhaa, wakiwamo wafanyakazi na viongozi 38 wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Pia tuhuma hizo zinawahusu baadhi ya watu walioweka taarifa batili kwenye mtandao, ikiwamo taarifa zinazodaiwa kuwa potofu, zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange. Ujenzi wa Viwanda na Hospitali. Dk. Magufuli alikuwa akiahidi katika kampeni zake kuwa atajenga viwanda katika kila mkoa, kulingana na mahitaji ya sehemu husika, ili kulifanya taifa lijitegemee na wakati huo huo, kuongeza fursa za ajira, jambo ambalo hajalitolea kauli tangu aingie madarakani. Ahadi nyingine ni kuhusu ujenzi wa zahanati katika kila kijiji, kituo cha afya katika kila kata, hospitali kwa wilaya zote na Hospitali ya Rufaa kwa kila mkoa. Hadi sasa mchakato wa kukamlisha ahadi hizo imebaki kuwa kimya. Changamoto ya amani na utulivu. Matukio ya ukosefu wa utulivu amani, kama vile vurugu kutawala kwenye matukio ya uchaguzi katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi, ni changamoto ya utawala mpya wa Rais Dk. Magufuli. Mojawapo ni tukio la Desemba 20, mjini Tanga katika uchaguzi wa Meya na naibu wake, zilitawaliwa na vurugu, hali kama hiyo nayo ilitiokea siku ya Desemba 10, mwaka huu katika kikao kama hicho, katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Kote Polisi walilazimika kuingilia kati. Ufanisi wa serikali yake. Rais Dk. Magufuli mara baada ya kuapishwa Novemba 5, siku hiyo hiyo alimteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, amsaidie majukumu ya msingi yaliyimkabili ndani ya muida mfupi. Siku moja baadaye, Novemba 6, alifanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha na Ofisini ya Hazina, kubaini uhalisia wa utendaji wa watumishi serikalini. Ilipofika Novemba 19, alimteua Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu, ambaye wamekuwa wakiendesha kampeni nzito katika safu ya timu moja. Desemba 3, mwaka huu, Rais alifanya kikao na jumuiya ya wafanyabiashara akiwaagiza wote wanaotuhumiwa kutoa mizigo yao bandarini bila ya kulipiwa kodi, walipe madeni yao ndani ya siku saba, kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa. Rais Dk. Magufuli, kwa akishirikiana na Waziri Mkuu Majaliwa, walisaidia kukamatwa kwa makontena tisa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) eneo la Mbezi, Tangibovu yakiwa yametoroshwa bila kulipiwa ushuru wa Sh. milioni 58. Kubana matumizi. Siku ya Novemba 7, Rais Magufuli alifanya kikao na watumishi wa serikali, wakiwamo makatibu wakuu wa wizara na naibu wao, pia watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali za umma, kujadili hoja ya namna ya kufanya kazi kwa ufanisi katika serikali yake. Dk. Magufuli aliwatangazia watumishi hao kufutwa safari za nje za watumishi mpaka pale atakapotoa tena tamko au kwa ridhaa yake. Alichukua uamuzi wa kufuta safari hizo baada ya kubaini kuwapo kwa matumizi makubwa ya fedha kwa watumishi wa serikali, walioko katika taasisi, wizara na idara za serikali ambao walikuwa wakijipangia safari bila ya utaratibu maalum. Pia, Rais Magufuli Novemba 23, alitangaza kufuta Sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara, ukiotakiwa kufanyika Desemba 9 na akaagiza itumike kusafisha mazingira, tukio lililofanyika kwa mafanikio makubwa. Inaelezwa kuwa, uamuzi huo iliokoa kiasi cha Sh. bilioni nne ambazo zingetumika kwa sherehe hizo na zikahamishiwa katika mradi wa ujenzi wa upanuzi wa barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, kipande cha Morocco - Mwenge. Pia katika hatua hiyo hiyo ya kubana matumizi, Rais Dk. Magufuli amefuta matumizi holela ya fedha za umma katika ununuzi wa kadi za sikukuu na samani za ofisi kutoka nje ya nchi. Katika tukuio lingine lililovutia umma ni la Novemba 20, mwaka huu Rais Dk. Magufuli aliagiza fedha zaidi ya milioni Sh. 225 zilizokuwa zitumike katika sherehe za kufungua bunge mjini Dodomam, zielekezwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kufanya maboresho ya huduma. Siku tano baadaye, Novemba 25, mwaka huu, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alitangaza kufutwa kwa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani nchini, akaelekeza bajeti ya sherehe hizo zitumike kununua dawa za kufubaza makali ya Ukimwi (ARVs). Maamuzi magumu. Novemba 9, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako alikuta hali mbaya ya huduma, huku baadhi ya mashine muhimu za vipimo ikiwamo CT Scan havifanyi kazi kwa miezi kadhaa. Ni tukio liliooendana na kufutwa kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Hospitali hiyo na kuuondolewa kwa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk.Hussein Kidanto, aliyejeshwa katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnia,Wazee na Watoto. Katika ziara hiyo, Rais Magufuli aliagiza mashine za vipimo za MRI na CT-Scan zitengenezwe mara moja kwa kutolewa kiasi cha Sh. bilioni 3 kugharimia matengenezo hayo, huku akiamuru mgonjwa aliyetelekezwa kwa miezi zaidi ya miwili, atibiwe mara moja. Baadaye, Novemba 27, mwaka huu, alihamia katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kumsimisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade. Ilikuwa ni baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini upotevu wa makontena 349, yaliyotolewa bandarini bila ya kulipiwa ushuru na kuisababishia serikali kukosa mapato yake ya Sh. bilioni 80. Desemba 7, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli pia alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadhi Massawe, kisha akaivuja Bodi yake Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), iliyokuwa chini ya Profesa Joseph Msambichaka. Hali kadhalika, Desemba 16, mwaka huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, akitoa sababu ya kutoridhishwa na utendaji wa taasisi yake, katika kasi kukabiliana na rushwa nchini. Ni hatua iliyoendana na kufutwa kazi kwa watumishi wanne wa Takukuru, aliosema walikaidi agizo la kutoruhusiwa kwenda nje ya nchi, pasipo kibali cha mamlaka inayowasimamia. Juzi, Rais aliendeleza pamnga lake hilo, kwa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito, akitaka apishe uchunguzi wam, kuhusu tuhuma za kukiuka taratibu za manunuzi ya umma, katika mchakato wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati. Ahadi alizozitekeleza. Rais Magufuli wakati akifanya kampeni za urais alitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi kuwa angezitekeleza mara tu atakapoingia madarakani. Mojawapo ya ahadi ambayo ameshaitekeleza tangu aingine madarakani ni utoaji wa elimu bure kuangia elimu ya msingi hadi sekondari kuanzia mwaka 2016/17 hatua ambayo imeshaanza kutekelezwa na baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya. Ahadi nyingine ni kuwaajibisha watendaji wazembe serikalini kwa kuwafukuza kazi bila ya kuwaamisha vituo vyao vya kazi kama ilivyozoeleka kwa watangulizi wake walivyokuwa wanafanya. Kutekeleza hilo, Rais Magufuli ameshamsimamisha kazi Dk. Edward Hoseah wa Takukuru, Kamishna wa TRA, Rashed Bade, Mkurugenzi wa TPA, Awadhi Massawe na Mkurugenzi wa Rahco, Mhandisi Benhadard Tito. Kadhalika, Rais Magufuli ameshaanza kutekeleza ahadi ya kuongeza makusanyo ya mapato kutoka bilioni 800 hadi kufikia trilioni moja, kwani kwa muda wa siku 30 aliweza kukusanya mapato yanayokadiriwa kufikia Sh. trilioni 1.3. Kimataifa. Tangu aingie madarakani, Rais Dk. Magufuli amekuwa gumzo katika nchi mbalimbali duniani, ikiwamo Afrika, Ulaya na Marekani. Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Independent la Afrika Kusini, ilibeba tahariri ya kimataifa yenye kichwa cha manenio yanayomsifia Dk. Magufuli ” Afrika ifuate mfano wa Tanzania.” Sehemu ya tahariri hiyo ilikuwa na maelezo: “Afrika inahitaji Rais kama Dk. Magufuli, ambaye ameonyesha kwa dhati, nidhamu katika matumizi ya serikali.” Pia, nchi za Ghana na China nazo zimejitokeza kusifu uchapakazi wa Rais Magufuli. Nchini Kenya, wananchi wake nao wamekuwa wakitaka serikali yao iwe na mfumo kuwajibika kwa mfano wa utendaji wa Rais Dk. Magufuli, huku katika katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Uganda, mgombea mmoja alijinadi kwa kudai auchaguliwe, ili achape kazi kwa mfano wa Rais Dk. Magufuli.
CHANZO: NIPASHE
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
Friday, December 25, 2015
HAPA KAZI TUU:-Mambo 6 pasua kichwa siku 50 za Magufuli leo December 25,2015.
Tags
# HABARI
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment