Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi Angelina Mabula
Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi Angelina Mabula amefanya ziara ya
kushtukiza Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam na kukuta zaidi ya nusu ya watendaji wake wako likizo.
Naibu Waziri
huyo aliwasili ofisini hapo jana saa 8.30 mchana na kupokewa na mtunza
kumbukumbu, Bahati Kassim ambaye ni mtumishi pekee aliyekuwapo ofisini.
Baada ya
kusaini kitabu cha wageni, naibu waziri aliuliza waliko watumishi wengine.
Naibu
Waziri: Watumishi wengine wako wapi?
Bahati: Wako
likizo na mmoja ametoka kikazi.
Naibu
Waziri: Baraza lina watumishi wangapi hapa Kinondoni.
Bahati: Tupo
watumishi sita.
Naibu
Waziri: Wangapi wako likizo.
Bahati:
Wanne, tumebaki wawili, mmoja ambaye ni mwenyekiti ametoka ana kazi za nje.
Baada ya
kujibiwa hivyo, Mabura alisema haiwezekani watumishi wanne wakawa likizo kwa
wakati mmoja, wakati baraza lina watumishi sita.
“Kuna
mpangilio mbaya wa likizo, hii ina maana kuna siku ofisi zitafungwa kwa sababu
watumishi mtakuwa likizo,” alisema.
Mtunza
kumbukumbu pia alimueleza kati ya mwaka 2004 hadi sasa, kuna kesi zaidi ya
2,000 zilizofikishwa mbele ya baraza hilo na kati ya Januari hadi sasa,
wamepokea kesi 300.
Awali,
Mabula alitembelea kijiji cha King’azi kinachogombewa na wilaya za Kisarawe na
Kinondoni ambako aliunda timu ya wataalam watakaochunguza mipaka ya vijiji vya
King’azi, Msopwa na Mloganzila ili kubaini viko upande gani.SOURCE:-MWANANCHI.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
Wednesday, December 30, 2015
HAPA KAZI TU:-Waziri akuta ‘ofisi nzima’ wako likizo.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment