RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amevunja bodi ya
Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa
Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe.
Kuvunjwa kwa
bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu na
kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo,December 07,2015,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kunatokana na
ziara alizofanya katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini uwepo wa mianya ya
ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na
Septemba mwaka jana,2014.
Amesema
upotevu huo unatokana na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo ambao unatoa
mwanya wa kupoteza mapato ya serikali na kutaka mfumo huo ubadilishe kufikia
Desemba 11.
Waziri Mkuu,
Majaliwa amesema kuwa kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu, ripoti
iliwataja waliohusika na upitishaji wa makontena hayo na bila ya kuwepo kwa
taarifa yeyote, hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa Bandari Kavu (ICD)
ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike,
Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante pamoja na James Kamwomwa.
Wengine
ambao hakuwemo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa
makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ambao ni Shaban
Mngazija Aliyekuwa Meneja Mapato, Rajab
Mdoe Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu, Ibin Masoud Kaimu Mkurugenzi
wa Fedha ,Apolonia Mosha Meneja wa Bandari Msaidizi (Fedha).
Waziri Mkuu,
amesema kuwa katika ziara yake kwa
Shirika la Reli Nchini (TRL) alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13
nje ya utaratibu ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika.
|
No comments:
Post a Comment