Leo Desember 05,2015 huko Addis Ababa Nchini
Ethiopia, Rwanda na Uganda zimecheza Fainali ya Kombe la Chalenji ambazo Mshindi
wake hubeba Kombe linaloashiria ndio Nchi Bingwa ya Afrika Mashariki nay a Kati
na pia kuzoa kitita cha Dola 30,000.
Timu itakayoibuka mshindi wa pili
katika Fainali hii itapewa Dola 20,000.
Rwanda ilitinga Fainali hii baada ya
kutoka 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo na Sudan na kushinda kwa Penati wakati
Uganda pia ilikwenda Sare 0-0 na Wenyeji katika Dakika Uganda ‘The Cranes’ wameibuka mabingwa wa
michuano ya Chalenji iliyomalizika leo nchini Ethiopia.
Katika fainali hiyo-UGANDA
wamefanikiwa kutwaa taji la 14 la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Challenge CUP 2015 baada ya kuifunga Rwanda bao 1-0 jioni ya leo nchini
Ethiopia katika mchezo wa fainali.
Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo
pekee, Ceasar Okhuti aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Dennis Okot kwa kumtungua
Eric Ndayishimiye dakika ya 15.
Kocha Mserbia Milutin ‘Micho’
Sredojevic ambaye amewahi kuifundisha Rwanda alikuwa mwenye furaha na akasema
Uganda imedhihirisha ubora wake katika ukanda wa CECAFA.
Safu ya ilinzi ya Uganda ilikuwa
inaongozwa na beki wa Simba, Juuko Murishid ambaye ameingoza timu hiyo kubebwa
ubingwa dhidi ya Rwanda ambayo ilikuwa na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzoma na
kiungo wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza.
“NInafurahia
kazi, ni furaha kubwa, tumedhihirisha sisi ni bora katika ukanda huu, tukiwa
timu pekee iliyofuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018
Urusi, na tunabeba Kombe la Challenge,”amesema.
Mapema katika mchezo uliotangulia, wenyeji
Ethiopia walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Sudan kwa penalti 5- 4
kufuatia sare ya 1-1.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
| | | |
No comments:
Post a Comment