Wanakijiji
wa kijiji cha Shenda wilayani Geita wakiongea na waandishi wa habari
waliotembelea kijiji hicho ambapo walilalamikia
kutupwa kwa takataka katika kijiji hicho siku ya tarehe 9 ambapo ilikuwa
siku ya usafi kwa nchi nzima
Krantz
Mwantepele,Geita
Wananchi wa
kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita
Wameitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka
zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9,2015 Lililofanyika
nchi nzima.
Wakiongea na
waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa
wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutupa takataka katika
kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.
Wameongeza
kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule
ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya
kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza na kusambaa
katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.
Sambamba na
hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri kutupa taka
hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo
yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji
chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.
Kwa mujibu
wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda amesema sehemu zilizotupwa
taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza kuhusu hatua hiyo waliambiwa
kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu hiyo na ndipo walipoamua kutupa
taka hizo.
Kwa upande
wake Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe…………..amesema kuwa baada ya
wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu katika taka hizo na
kwamba hawajaziamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment