TAZAMA PICHA:-Namna Jeshi la Polisi likitoa Elimu kwa Abiria na Madereva ili kudhibiti Ajali mwishoni mwa Mwaka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 10, 2015

TAZAMA PICHA:-Namna Jeshi la Polisi likitoa Elimu kwa Abiria na Madereva ili kudhibiti Ajali mwishoni mwa Mwaka.

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Koplo Abdallah Bwasi akikagua moja ya magari yanayofanya safari zake nje ya mkoa wa Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam.Hatua hii ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani imekuja kwa lengo la kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Sajenti Jackson Mafuru (kulia), na PC Elisante Bura(kushoto), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani. zoezi hili ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam, ni moja ya hatua ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Swami(aliyeko chini ya uvungu wa gari), akikagua moja ya magari yanayojiandaa kuelekea mikoani, zoezi ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuanza kuondoka katika kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam.aliyenyoosha kidole juu ni PC Elisante Bura. Hatua hii ya Jeshi la Polisi nchini linalenga kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Samwi(kushoto), na PC Elisante Bura(kulia), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani, kutekeleza mkakati wa Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.Zoezi hili limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Asha Adam, akiwasisitiza abiria kufunga mikanda iliyopo kwenye viti walivyoketi muda wote wa safari muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi ya abiria Ubungo, jijini Dar es Salaam, kama hatua ya kudhibiti majeraha na vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Makao Makuu ya Trafiki, Dar es Salaam, ASP Abel Swai akitoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria, muda mfupi kabla ya kuanza safari za mikoani katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo, jijini Dar es Salaam, elimu ambayo inalenga kudhibiti ajali za barabarani kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad