Mmshambuliaji
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif
‘King Kibaden’ Pichani , ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro
Stars itakayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Challenge 2015 nchini Ethiopia.
Tukiwa
bado akili na macho ya watanzania wengi yapo katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi, ambapo Taifa Stars
itacheza mechi ya kwanza na Algeria November 14 uwanja wa Taifa Dar
Es Salaam, shirikisho la soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limetangaza
Makundi matatu ya timu zitakazocheza michuano ya Challenge inayotarajia
kuanza November 21 na kumalizika December 6,2015.
KUNDI A
1.
Ethiopia
2.
Tanzania
bara
3.
Zambia
4.
Somalia
KUNDI B
1.
Burundi
2.
Djibouti
3.
Kenya
4.
Uganda
KUNDI C
1.
Rwanda
2.
Sudan
3.
Sudan
Kusini
4.
Zanzibar
Timu ya taifa ya Kenya ndio
Mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo walitwaa mara ya mwisho mwaka 2013 Nairobi
kwa kuifunga Sudan.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment