Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Donan Mmbando, leo jijini Dar es Salaam.
|
Wadau
mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo
jijini Dar es Salaam
(Picha na
Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii.
MLIPUKO wa
Ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika mikoa 14 na kufikia wagonjwa 7,825 na vifo 106.
Akizungumza
na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Donan Mmbando amesema kati ya wagonjwa wote waliougua 3746
sawa na asilimia 67 wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema
kuwa Mikoa inayotoa taarifa ya kuwepo
wagonjwa wapya ni Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mara,
Singida na Tanga.
Mmbando amesema kuwa ugonjwa huo umeripotiwa katika mikoa mingine
ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Pwani, Singida, Mara, Arusha, Tanga, Mwanza,
Shinyanga, Morogoro, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma, Kigoma, Geita pamoja na
Rukwa.
Aidha
amesema hadi kufikia Novemba 8,2015
idadi ya wagonjwa waliokwisha kuripotiwa tangu mlipuko uanze hapa nchini
ni 7825 na vifo 106 amabo ni asilimia 1.3 ya waliougua.
Amesema
hatua walizozichukua kwa ugonjwa huo ni kutoa dawa, vifaa vya maabara na vifaa
kinga kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro.
Aliongeza
kuwa Wizara imepokea maombi kutoka mikoa
ya Singida, Arusha, Tanga, Mwanza, Mara na Geita kati ya Oktoba 15 mwaka
huu,2015 na yanashughukuliwa na utawala,
Kupima vipimo vya maabara na kufuatilia ubora wa vipimo kutoka katika mikoa
iliyofanya uchunguzi na kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo, Kupeleka timu za
watalaam kutoka ngazi ya Mkoa na Taifa kusaidiana na timu za Wilaya husika.
Aidha tarehe
28 Oktoba 2015, Timu ya Kitaifa ilienda katika mikoa ya Tanga, na Singida na
vilevile mkoa wa Manyara pia timu ilienda kwa ajili ya kufuatilia tarifa za
kuwepo kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika – taarifa ya timu hizi inakamilishwa
na itawasilishwa.
Mmbando
amesema hatua nyingine Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya ufuatiliaji
wa ugonjwa na utoaji wa matibabu ,Kutoa elimu ya kwa umma kupitia vyombo vya
habari hususani radio na runinga.
Aidha, mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali vya habari nchini yametolewa, Kuandaa “Water safety plan” kwa
kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo WHO, PSI, CDC, MSF, Redcross na USAID.
Aidha mpango mkatati huu utajikita kwanza kwa jiji la Dar es salaam kwa kuanzia
na hapo baadae itaenda katika mikoa mingine.
Amesema
changamoto katika ugonjwa huo ni,Mwitikio hafifu wa jamii juu ya kukabiliana na
ugonjwa huu,Jamii kutokuzingatia kanuni za afya na mazingira,Ushiriki mdogo wa
sekta nyingine katika kupambana na ugonjwa huu,Ukosefu wa pesa za kuwalipa
watumishi wa afya wanaohusika katika zoezi la kukabiliana na ugonjwa huu.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment